KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, February 14, 2014

Safari ya Twiga Stars kuelekea fainali za mataifa ya Afrika kwa wanawake nchini Namibia yaanza kwa kufungwa bao 2-1 uwanja wa Nkoloma jijini Lusaka

Safari ya kuelekea kwenye fainali za 9 za mataifa ya ya Afrika kwa soka la wanawake (AWC) nchini Namibia 2014 zimeanza kwa raundi ya kwanza michezo yake kuanza kupigwa barani Afrika.

Jumla ya timu kumi na sita zimekuwa zikihusika kusaka nafasi katika fainali hizo kote barani humu ambapo kuna nafasi saba tu za kushindaniwa ambapo wataungana na mwenyeji wa fainali hizo Namibia zitakazo pigwa kuanzia mwezi Oktoba ambapo pia watapatikana wale waliofuzu kwa ajili ya fainali za kombe la dunia mwakani 2015 nchini Canada.



Katika dimba la Nkoloma Stadium jijini Lusaka, timu ya taifa ya wanawake ya Zambia maarufu kama 'She-polopolo' walikuwa wenyeji wa Twiga Stars ya Tanzania. 

 Twiga Stars wamepoteza mchezo kwa kuchapwa bao 2-1 ambapo mpaka kufikia mapumziko mchezo huo ulikuwa na matokeo ya sare ya bila kufungana.

Wazambia wameingia kwenye mchezo huo wakiwa na dhamira ya kutinga fainali za michuano hiyo kwa mara ya kwanza lakini wakikumbana na timu bora ya wanawake kutoka ukanda wa soka wa Afrika Mashariki na kati timu ya Twiga stars. 

Zambia pia waliiingia katika mchezo huo wakiwa na nguvu ya kutosha na ambayo imewasukuma kupata matokeo mazuri kufuatia vijana wenye umri chini ya miaka 17 wa nchi hiyo kuweka historia kwa kufuzu fainali za kombe la dunia kwa wachezaji wa umri huo ambazo fainali zake zitafanyika nchini Costa Rica.
 
Nchini Burkina Faso katika jiji la Ouagadougou hapo kesho wenyeji hao maarufu kama ‘Les Etalons Filles’ watakuwa wakiwakaribisha majirani zao Black Queens ya Ghana huku wakiwa na dhamira ya kufanya kweli na kutinga katika fainali ya mwaka huu baada ya kushindwa katika fainali zilizopita ambazo zilifanyika Equatorial Guinea mwaka 2012.

Black Queens ambazo wamekuwa washindi wa pili mara tatu katika fainali zilizopita watakuwa katika dhamira ya kujenga hadhi yao barani humu wakiwa chini ya kocha Yusif Basigie, ambaye alipewa dhamana ya kuhakikisha bahati inakuwa upande wao safari hii.



‘Les Elephantes’ ya Cote d’Ivoire wameewaalika Mali katika uwanja wa Robert Champroux mjini Abidjan, huku kocha wa kikosi hicho Clementine Toure akitaraji kupata ushindi kama ule walioupata katika mchezo wa majaribio dhidi ya timu ngumu ya soka la wanawake ya nchini humo ya Juventus de Yopougon na kutumia nguvu hiyo kuwadhoofisha Mali.

Mjini Gaborone, Botswana itakuwa wenyeji wa Zimbabwe katika mchezo ambao unawakutanisha timu mbili kutoka ukanda mmoja wa kisoka yaani Afrika kusini. Botswana watakuwa na nguvu zaidi kufuatia ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Swaziland katika mchezo wa kujipima nguvu wiki iliyopota huku kocha wake Mmoloki Masele akitamba kikosi chake kimekuwa tayari kwa changamoto ya michuano hiyo na akianza na Zimbabwe.

Wao Zimbabwe maarufu kama Mighty Warriors walifanya ziara ya maandalizi yao nchini Misri ambapo walicheza michezo kadhaa na kupata matokeo ya kushinda 2-1 na kufungwa 3-2 dhidi ya Misri katika michezo miwili ya kujipima nguvu mjini Cairo. 

Kocha wa Zimbabwe mwanamama Rosemary Mugadza, amesema michezo miwili waliyocheza dhidi ya Misri imewaweka katika nafasi nzuri ya kuanza michezo hiyo ya kuwani kufuzu fainali za Afrika baadaye mwaka huu.

Mjini Kigali, Rwanda watakuwa wenyeji wa Kenya ambapo kocha wa Rwanda mwanamama Grace Nyinawumuntu, akitaraji kupata ushindi katika mchezo.

Amenukuliwa na Rwandan News Times akisema

“Mchezo dhidi ya Kenya ni muhimu sana kwetu na tumejiandaa vya kutosha. Tunapaswa kushinda ili kujitengenezea nafasi nzuri ya kufuzu. Tunataka kuwa ni miongoni mwa timu bora barani Afrika na tunajua tunaweza, tutafanya kazi kubwa na kujiandaa vema kwa kadri ya uwezo wetu.

Afrika ya kaskazini vigogo Misri na Tunisia watakuwa wakipambana mjini Cairo, ilhali Algeria watakuwa wenyeji wa Morocco katika uwanja wa Omar Hamadi mjini Algiers hii leo.

Michezo ya pili ya marudiani itapigwa kuanzia Februari 28 mpaka March 2 mwaka huu 2014 ambapo washindi wa matokeo ya jumla wataungana na bingwa mtetezi Equatorial Guinea, South Africa na Cameroon katika raundi ya pili, ambao hawakuhusika na michezo ya roundi ya kwanza

14/2/2014 Algeria vs Morocco
15/2/2014 Zambia vs Tanzania
15/2/2014 Burkina Faso vs Ghana
15/2/2014 Cote d’Ivoire vs Mali
16/2/2014 Egypt vs Tunisia
16/2/2014 Rwanda vs Kenya
16/2/2014 Botswana vs Zimbabwe

Nigeria vs Sierra Leone*
Ethiopia vs South Sudan*
*Mozambique vs Comoros
*Guinea Bissau vs Senegal

No comments:

Post a Comment