KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, February 15, 2014

YANGA YAFUZU HATUA YA PILI, YAICHAPA KOMOROZINE de DOMONI 5 -2, NGASA ATUPIA HAT-TRICK

Wafungaji wa magoli ya Yanga ya leo hapa wakiwa katika picha katika mchezo wa kwanza iliyopigwa uwanja wa Taifa.
  Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya vilabu bingwa barani Afrika Yanga ya jijini Dar es Salaam hii leo imeibuka na ushindi mwingine mnono dhidi
Komorozine de Domoni ya Comoro kwa ushindi wa mabao 5-2 katika mchezo uliochezwa uwanja wa Sheikh Said Ibrahim Mitsamihuli huko Anjuani Comoro.
Mrisho Khalfani Ngasa ndiye aliyekuwa mwiba mkali kwa wacomoro kwa mara nyingine tena akifunga magoli matatu peke yake yaani Hat-trick kwa mara nyingine tena.
Ngasa amefunga magoli yake matatu katika dakika za 22,87 na 90 huku mabao mabao mengine yakifungwa na Hamisi Diego Kiiza likiwa ni bao la kwanza kunako dakika ya 13 ya mchezo huku Simon Msuva akiaandika bao lake kunako dakika ya 37 ambalo lilikuwa ni bao la tatu kwa Yanga.
Itakumbukwa katika mchezo wa kwanza uliochezwa uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 7-0 na hivyo kuifanya Yanga kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa mabao 12-2 wakiwasubiri AL Ahly ya Misri.
Ikicheza mbele ya Balozi wa Tanzania nchini Comoro Bw. Chabaka Kilumanga Young Africans imefanikiwa kufuzu hatua ya pili ya Mashindano ya Klabu Bingwa Barani Afrika kwa jumla ya mabao 12- 2, kufutaia ushindi wa mabao 7-0 katika mchezo wa awali uliofanyika jijini Dar es salaam huku Mrisho Ngasa akifunga "Hat-trick" katika michezo yote miwili.
Komorozine de Domoni ikicheza mbele ya Gavana wa jimbo lao la Anjuani iliuanza mchezo kwa kasi kwa lengo la kusaka bao la mapema ili kuwapa nguvu washangiliaji wao amabo walikuja kuipa sapoti timu hiyo.
Hamis Kiiza aliipatia Young Africans bao la kwanza dakika ya 13 ya mchezo kufuatia kuitumia vizuri krosi ya mlinzi wa kushoto Oscar Joshua aliyepanda kuongeza nguvu mashambulizi na pasi yake kumkuta Kiiza ambaye aliukwamisha mpira wavuni bila ajizi.
Dakika ya 22 ya mchezo, Mrisho Ngasa aliwainua mashabiki wa Young Africans vitini kufuatia kuifungia timu yake bao la pili kufuatia migongeo mizuri ya Haruna Niyonzima na Didier Kavumbagu.
Saimon Msuva aliipatia Young Africans bao tatu kufuatia kufanya shambulizi langoni mwa timu ya Komorozine de Domoni baada ya pasi za viungo Athuman idd, Haruna Niyonzima na Mrisho Ngasa kumkuta mfungaji ambaye hakufanya makosa.
Dakika ya 41 ya mchezo makosa ya mpira ulioptezwa na Hamis Kiziza yaliwapelekea Komorozine de Domoni kijipatia bao la kwanza baada ya mshmabuliaji wao kumtoka Oscar Joshua na kupiga krosi iliyomkuta mfungaji.
Dakika 45 za kipindi cha kwanza zilimalizika, Komorozine de Domoni 1 - 3 Young Africans.
Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko ambapo Young Africans iliwaingiza Frank Domayo, Hassan Dilunga na Said Bahanuzi waliochukua nafasi za Athuman Idd, Saimon Msuva na Didier Kavumbagu mabadiliko ambayo yaliongeza kasi ya mashambulizi.
Dakika ya 77 Korozine de Domoni walijipatia bao la pili kufuatia makosa ya kiungo Hassan Dilunga baada ya mpira alipoteza kunaswa na msahmbuliaji wa Komorozine na kuwazidi ujanja walinzi wa Young Africans na kuukwamisha mpira wavuni.
Mrisho Ngasa aliipatia Young Africans bao la nne dakika ya 87 ya mchezo kufuatia Said Bahanuzi kuwatoka walinzi wa Komorozine na kupiga krosi iliyomkuta Ngasa na kuukwamisha mpira wavuni kwa kifua.
Dakika ya 90 ya mchezo Mrisho Ngasa aliendelea kuwapa furaha tena washabiki wa Young Africans waliojitokeza uwanjani leo kuishangilia timu yao baada ya kuipatia timu yake bao la tano na la ushindi kwa kichwa baada ya kuitendea vyema krosi ya kiungo Haruna Niyonzima.
Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika, Komorozine de Domoni 2 - 5 Young Africans.
Mara baada ya mchezo mwamuzi wa mchezo wa leo Allister Barra alimkabidhi mpira mshambuliaji Mrisho Ngasa kufuatia kufunga mabao 3 peke yake (hat-trick) katika mchezo wa leo.
Baadhi ya watanzania walijitokeza kuishangilia timu yao ya Young Africans wakiongozwa na Balozi wa Tanzania nchini Comoro Chibaka Kilumanga  walifurahishwa na ushindi huo na kusema wamefarijika na timu yao kwa kushinda mchezo wa leo na kusema wanaitakia kila la kheri katika michezo inayofuata.
Kesho mchana Msafara wa Young Africans umealikwa chakula cha mchana nyumbani kwa Balozi wa Tanzania nchini Comoro Bw.Ckibaka Kilumanaga  na siku ya jumatatu kikosi kitaanza safari ya kurejea nchini majira ya saa 6 mchana kwa shirika la ndege Precision Air.
Young Africans: 1.Dida, 2.Twite, 3.Oscar, 4.Cannavaro, 5.Yondani, 6.Chuji/Dilunga, 7.Msuva/Domayo, 8.Niyonzima, 9.Didier/Bahanuzi, 10.Ngasa, Kiiza

No comments:

Post a Comment