Wakati Baecelona ikikabiliwa na mchezo mwingine wa ligi kuu ya nchni Hispania Jumapili dhidi ya Atletico Bilbao, inaarifiwa kuwa klabu hiyo inabailiwa na hali mbaya.
Siku nane zilizopita, Lionel Messi na wenzake ndani ya kikosi cha Barca walikuwa katika nusu
fainali ya Champions League, pointi moja nyuma ya Atletico Madrid katika
La Liga, na ikijiandaa kwa fainali ya Kombe la Mfalme dhidi ya Real
Madrid.
Sio kawaida kwamba timu kubwa ya soka Ulaya husambaratika haraka sana,
kama vile Barcelona ilivyofanya wiki hii. Ni kweli, ulikuwa msimu mgumu
kwa Barca, Tito Vilanova kujiuzulu mwezi Julai kama kocha kutokana na
saratani ya koo, rais wa klabu Sandro Rosell kujiuzulu Januari kutokana
na kashifa ya usajili wa Neymar.
Lakini shida hizi zingewekwa kando
angalau washinde taji hata moja au mawili hali ambayo ingeipa klabu hiyo
utulivu.
Lakini kikosi hicho cha kocha Gerardo Martino kimechimba chini
katika wakati mbaya huku safu ya ulinzi ikikabiliwa na majeruhi chungu
nzima, nayo ya kiungo ikiyumbayumba, huku mashambulizi ya ushirikiano wa
Neymar na Messi yakiwa butu na yanayotabirika.
Barca waliondolewa nje ya Champions League kwa kushindwa na Atletico
Madrid, na sasa wako nyuma ya viongozi hao Atletico katika nafasi ya
tatu kwenye la liga, jambo ambalo linafanya iwe vigumu kwa vijana hao
kutetea taji hilo.
Na kukamilisha wiki yenye masaibu, barca walifungwa na Real Madrid
magoli mawili kwa moja dhidi ya Real MADRID katika fainali ya Kombe la
Mfalme. Nini kinachofuata?
Wengi bila shaka wanataka mageuzi makubwa katika kikosi hicho kuanzia
kwa kocha. Kwa mujibu wa vyombo vya habari majina yanayopigiwa upatu
kuchukua ungozi wa Camp Nou ni kocha wa Borussia Dortmund Jurgen Klopp.
Hayo bila shaka tutasubiri kuona namna yatakavyokwenda.
Kwa upande wake Lionel Messi anaamini kuwa Barcelona kwasasa wanamuona yeye kama bidhaa na kwamba si mchezaji aliyekuwa ashikiki tena kwa gharama, hizi zikiwa ni taarifa zilizoripotiwa kwenye chaneli maarufu inayojulikana kama Catalan sports channel Esport3.
Mapendekezo yanaonyesha kuwa bodi ya klabu hiyo inaamini kuwa mchezaji huyo anathamani zaidi kwa mpango wa uhamisho yaani 'transfer market' kuliko anapokuwa uwanjani kitu ambacho kimemuweka Messi katika mkao wa matayarisho ya kuondoka Katalunya.
No comments:
Post a Comment