Mkurugenzi wa ufundi wa TFF Salum Madadi ambaye pia ni kocha mkuu wa muda wa timu ya taifa 'Taifa Stars'. |
Wachezaji
wazoefu wa Taifa Stars watakaoungana na wale 16 waliopatikana katika mpango wa
maboresho wa timu hiyo watatangazwa kesho (Aprili 19 mwaka huu) saa 4 asubuhi
kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Taifa
Stars itapiga kambi kwenye hoteli
ya Kunduchi Beach kujiandaa kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Burundi
itakayochezwa Aprili 26 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Salum Mayanga |
Jana katika ukumbi wa Hoteli ya Hill View iliyopo mjini Tukuyu kocha msaidizi wa kikosi cha timu ya taifa cha maboresho Salum
Mayanga, alitangaza jumla ya majina 16 ya wachezaji waliochujwa na kujiunga na kikosi cha wachezaji wengine wazoefu watakao piga kambi kwa mchezo dhidi ya Burundi.
Wachezaji
hao ni kipa Benedicto Tinoko Simwanda (Mara), Emma Namwondo Simwanda (Temeke), Joram
Nason Mgeveje (Iringa), Omari Ally Kindamba (Temeke), Edward Peter Mayunga (Kaskazini
Pemba), Shiraz Abdallah Sozigwa (Ilala), Yusuf Suleiman Mlipili (Temeke) na Said
Juma Ally (Mjini Magharibi).
Wengine
ni Abubakar Ally Mohamed (Kusini Unguja), Hashim Ramadhan Magona (Shinyanga),
Omari Athumani Nyenje (Mtwara), Chunga Said Zito (Manyara), Mohammed Seif Saidi
(Kusini Pemba), Ayoub Kasim Lipati
(Ilala), Abdurahman Othman Ally (Mjini
Magharibi) na Paul Michael Bundara (Ilala).
No comments:
Post a Comment