LIGI Kuu ya soka Tanzania bara inafikia tamati
kesho (Aprili 19 mwaka huu) kwa timu zote 14 kuwa viwanjani, huku mabingwa wapya
Azam wakikabidhiwa kombe lao Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam katika mechi
yao dhidi ya JKT Ruvu.
Mechi
zote saba zitachezwa kuanzia saa 10 kamili jioni ambapo Yanga na Simba zitakuwa
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa mechi ambayo viingilio vyake ni sh. 7,000
kwa viti vya bluu na kijani, sh. 10,000 viti vya rangi ya chungwa, sh. 20,000
kwa VIP C na B wakati VIP A itakuwa sh. 30,000.
Taarifa ya shirikisho la soka nchini kupitia kwa ofisa habari na mawasiliano wa TFF Bonface Wambura imefanya marekebisho ya kiingilio cha chini cha mchezo wa watani wa jadi Simba na Yanga kutoka shilingi 5,000 na kuwa 7,000 huku viingilio vingine vikisalia kama vilivyo pangwa.
Tayari
tiketi za mchezo huo zimeanza kuuzwa leo (Aprili 18 mwaka huu) katika vituo saba vya; Shule
ya Sekondari Benjamin Mkapa, Kariakoo (Kidongo Chekundu), Buguruni Shell,
mgahawa wa Steers uliopo Mtaa wa Ohio na Samora, Ubungo OilCom, Dar Live
Mbagala na Uwanja wa Taifa.
Mechi
nyingine zitakuwa kati ya Tanzania Prisons na Ashanti United (Uwanja wa
Jamhuri, Morogoro), Rhino Rangers na Ruvu Shooting (Uwanja wa Ali Hassan
Mwinyi, Tabora), Mbeya City na Mgambo Shooting (Uwanja wa Sokoine, Mbeya), Oljoro
JKT na Mtibwa Sugar (Uwanja wa Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha) na Coastal
Union na Kagera Sugar (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga).
No comments:
Post a Comment