Kocha
Msaidizi wa Taifa Stars, Salum
Mayanga ametangaza majina ya
wachezaji 16 waliochaguliwa katika maboresho ya timu ya Taifa Taifa Stars
kwenye hoteli ya Hill View jijini Mbeya.
Wachezaji
hao ni kipa Benedicto Tinoko Simwanda (Temeke), mabeki wa kati; Emma Namwondo
Simwanda (Temeke) na Joram Nason Mgeveje (Iringa). Walinzi wa pembeni ni Omari
Ally Kindamba (Temeke), Edward Peter Mayunga (Kaskazini Pemba) na Shiraz
Abdallah Sozigwa (Ilala).
Viungo
ni Yusuf Suleiman Mlipili (Temeke), Said Juma Ally (Mjini Magharibi), Abubakar
Ally Mohamed (Kusini Unguja), Hashim Ramadhan Magona (Shinyanga), Omari
Athumani Nyenje (Mtwara) na Chunga Said Zito (Manyara).
Washambuliaji
ni Mohammed Seif Saidi (Kusini Pemba), Ayoub Kasim Lipati (Ilala), Abdurahman Othman Ally (Mjini
Magharibi), Paul Michael Bundara (Ilala).
Wachezaji wa U 20 ni Mbwana Mshindo
Musa (Tanga) na Bayaga Atanas Fabian
(Mbeya).
Alisema
mpango huu wa kuboresha timu ya Taifa ambayo inadhaminiwa na Kilimanjaro
Premium Lager ni endelevu na kusisitiza kuwa hata wale 18 walioachwa
watafuatiliwa na TFF na kuitwa panapokuwa na mahitaji.
“Hawa
wote wapo kwenye database ya TFF na hawataachwa tu hivi hivi wapotee,” alisema
kocha Mayanga.
Wachezaji
ha0 waliingia kambini mjini Tukuyu, Machi 21 mwaka huu na wamefanya mazoezi kwa
pamoja kwa karibu wiki nne sasa kabla ya kuchujwa.
Wachezaji
16 waliochaguliwa wanatarajiwa kuondoka Tukuyu kesho (Aprili 18 mwaka huu) na
kwenda kwenye kambi ya Taifa Stars katika Hoteli ya Kunduchi ambapo wataungana
na wachezaji wa Taifa Stars wa siku zote.
Baadaye
watachujwa tena ili ipatikane timu moja ya Taifa iliyoboreshwa.
Kampuni
ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Kilimanjro Premium Lager inaunga mkono
utaratibu huu wa maboresho ya Taifa na imewekeza zaidi ya dola milioni 2 kwa
mwaka kudhamini Taifa Stars. Huu ndio udhamini mkubwa zaidi ambao Stars imewahi
kupata tangu kuanzishwa kwa TFF.
LIGI YA MABINGWA WA MIKOA KUANZA MEI 10
Michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL)
itakayochezwa kwa ligi ya mkondo mmoja katika vituo vitatu vya timu tisa kila
kimoja inatarajia kuanza Mei 10 mwaka huu.
Timu ya kwanza kutoka katika kila kituo ndiyo
itakayopanda daraja kucheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu wa 2014/2015. Kwa
vile ligi hii haina mdhamini, hivyo timu zitajigharamia kwa kila kitu.
Vituo vitakavyotumika kwa ajili ya RCL, kanuni
pamoja na ratiba vitatangazwa kabla ya kuanza kwa ligi hiyo. Pia kituo
kitakachoteuliwa kwa ajili ya ligi hiyo, timu yake haitapangwa katika kituo
husika ikiwa ni moja ya njia ya kuhakikisha kanuni ya mchezo wa kiungwana (fair
play) inazingatiwa.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment