KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, April 17, 2014

Liverpool huenda wakamuongeza Mlinda mlango wa Ajaccio Guillermo Ochoa

Liverpool imepata faraja kubwa kuelekea kwenye kipindi cha uhamisho wa wachezaji kufuatia mlinda mlango Guillermo Ochoa aliyekuwa kwenye mpango wa usajili wao kudhihirisha kuwa angependelea kujiunga na ligi Englandt Premier League.

Mlinda mlango huyo wa Ajaccio amesema kuwa amekuwa akiwindwa na meneja wa wekundu wa England Brendan Rodgers, ambaye ana mtaka mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 28 akisubiri mkataba wake umalizike kiangazi.

Licha ya kuwepo na vilabu vingine kutoka nchini Italia ambavyo vimeonyesha nia, mlinda mlango huyo raia wa Mexico amesema anaendelea kufungua mawazo juu ya ofa mbalimbali.

‘Nachambua ofa kutoka mataifa mbalimbali, nimekuwepo Ufaransa kwa miak mitatu na napenda namna ilivyo, lakini nataka kujaribu sehemu nyingine’ amesema Ochoa.

‘Kwasasa sina makubaliano na timu yoyote na niko tayari kusikiliz maombi yote ili nifanye maamuzi sahihi.

‘Wakala wangu anashighulikia kila kitu na sija ondoa hatima yangu ya baadaye kwa Italia wala England.’

No comments:

Post a Comment