Ryan Giggs
ametangaza kustaafu kucheza mpira wa miguu ndani ya Manchester na kukamilisha career yake ya uchezaji soka kwa karibu robo karne.
Tangazo la Giggs linafuatia muda mfupi tuu baada ya klabu ya Manchester United kumtangaza kuwa namba mbili wa Louis van Gaal ndani ya Old Trafford hii leo Jumatatu.
Kipenzi hicho cha United ambacho kimeichezea klabu hiyo michezo 963 na kuitumikia timu yake ya taifa ya Wales mara 64
ametanabaisha kuning'iniza viatu vyake katika barua yake ya wazi kwa mashabiki wa klabu hiyo.
Ryan Giggs akishangilia goli lake katika mchezo wa pili wa nusu fainali ya michuano ya FA mwaka 1999 dhidi ya Arsenal, sasa amestaafu soka
Mkongwe wa Manchester United Ryan Giggs akielekea kukutana na Louis van Gaal mjini Holland wiki iliyopita
Picha ya mwaka 2008 ambapo Giggs anaonekana akishangilia kikombe cha European Cup, ndiye 'Manchester United's most decorated player'
Kazi mpya: Raia wa Weles atakuwa akimsaidia Van Gaal ndani ya Manchester United
Amekaririwa akiandika haya yafuatayo
'Ningependa kuchukua fursa hii kutangaza kustaafu kwangu kutoka katika soka la kulipwa na kuanza ukurasa mwingine katika maisha yangu kama meneja msaidizi wa Manchester United,' Giggs, mwenye umri wa miaka 40 amesema.
'Ninajivunia sana kuwa ni mwenye heshima ya kuichezea klabu hii kubwa duniani michezo 963 na Wales mara 64.'
Heshima ya Giggs ni pamoja na kushinda mataji 13 ya taji la 'Premier League' na mataji mawili ya ligi ya mabingwa.
Ameitumikia Man United kama kocha mchezaji karibu mwaka mzima uliopita na kuwa meneja wa muda katika michezo minne ya mwisho wa ligi kufuatia kufukuzwa kwa David Moyes.
United
imedhani kuna haja ya kumbakisha klabu hapo akitoa uzoefu wake katika nafasi ya ukocha na uwepo wake kwa baadaye unaaminika kuwa ni msaada kwa meneja mpya wa klabu hiyo Van Gaal.
Akinukuliwa zaidi Giggs amesema
'Ndoyo yangu siku zote ilikuwa ni kuichezea Manchester United, ingawa inanisikitisha kuwa sitakuwa nikivaa tena jezi kama mchezaji , lakini nimekuwa ni mwenye bahati kubwa kuikamilisha ndoto yangu kwa kucheza na wachezaji wakubwa sana duniani, kufanya kazi chini ya meneja mkubwa Sir Alex Ferguson, na zaidi ya hapo kucheza mbele ya mashabiki wa timu kubwa wa mpira wa miguu. Siku zote nimekuwa nikijali hili na naheshimu sapoti yenu'

MAISHA YA RYAN GIGGS NDANI YA OLD TRAFFORD
1973: Anazaliwa Ryan Joseph Wilson November 29 mjini Cardiff.
1990: Anasaini kuanza kufanya mazoezi Manchester United mwezi July na mwezi Disemba akianza kama 'professional'.
1991: Anaanza kutumia jina ubatizo Ryan Giggs.
Machi - Anaanza kuitumikia United kwa mchezo wa kwanza akiwa na umri wa miaka 17 akiingia akitokea benchi katika mchezo dhidi ya Everton. Miezi miwili baadaye anafunga goli la ushindi dhidi ya Manchester City mchezo uliopigwa Old Trafford.
October - Anakuwa mchezaji kijana kuiwakilisha Wales akicheza mchezo wa kimataifa dhidi ya Ujerumani mjini Nuremberg akiwa na umri wa miaka 17 na siku 322.
November - Anashinda taji la kwanza akiwa na United wakati United wakiwafunga Red Star Belgrade na kuchukua taji la UEFA Super Cup.
1992: Anaisaidia United kuchukua taji la League Cup na kushinda tunzo ya mwaka ya mchezaji kijana wa PFA.
1993: Anakuwa mchezaji wa kwanza kushinda wa kwanza kushinda tunzo mara mbili mfululizo wa PFA . Anakuwa pia ni miongoni mwa wachezaji wa kikosi cha United waliweka historia ya kushinda taji la Ligi.
1994: Anaisaidia United kushinda Premier League na FA Cup kwa mpigo.
1996: Anaisadia United kushinda mataji mawili kwa mara ya pili.
1997: Anashinda taji la tatu la ligi katika kipindi cha miaka minne na mwaka wa wanne huku pia mwezi Oktoba akifunga goli muhimu la ushindi katika ushindi wa magoli 3-2 katika michuano ya vilabu bingwa Ulaya dhidi ya Juventus mchezo uliopigwa Old Trafford.
1999: Alifunga goli zuri katika mchezo wa nusu fainali ya FA ukiwa ni mchezo wa marudiano dhidi ya Arsenal mchezo uliopigwa Villa Park mwezi Aprili mwaka huo. Anaisaidia United kukamilisha kukamilisha ushindi wa kihistoria wa mataji matatu ndani ya mwaka mmoja. (Champions League, Premier League and FA Cup trophies.)
2000:Anashinda taji la sita la Premier League ikiwa ni mwaka wake wa nane ndani ya Old Trafford.
2001: Anachukua taji la saba la ligi likiwa pia ni taji lake la 12.
July - Anasaini mkataba mwingine wa miaka mitano kuendelea kuitumikia Old Trafford.
2002: August 23: anafunga goli lake la 100 akiwa na United likiwa ni goli la pili timu katika mchezo wa ligi dhidi ya Chelsea.
2003: May - United wanatawazwa mabingwa wa ligi tena.
2004: May - United inamaliza ligi katika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi hiyo, huku Giggs akipangwa katika kikosi cha ushindi wa mabao 3-0 wa fainali ya FA dhidi ya Millwall.
2007: May 6 - Anashinda taji la tisa la 'Premier League' akiwa na Manchester United.
May 30 Anatangaza kustaafu kutoka katika soka la kimataifa.
December 11 - Anapokea tuzo ya OBE kutoka kwa Queen kwa utmishi wake katika mpira wa miguu.
2008: May 11 - Anaifikia rekodi ya Sir Bobby Charlton ya kucheza michezo 758 katika mchezo dhidi ua Wigan.
May 21 - Anaivunja sasa rekodi hiyo ya Charlton akiingia uwanja kama mchezaji wa akiba na kufunga goli la penati wakati Manchester United wakiwafunga Chelsea katika fainali ua ligi ya mabingwa Ulaya.
2009: April 26 - Anatajwa kuwa mshindi wa tuzo ya PFA(Professional Footballers' Association).
May 16 - Anaisaidia United kushinda taji la 'Premier League' na kuwa mchezaji wa kwanza kukusanya mataji 11 ya 'top division English league'.
December 13 - Anatajwa kuwa 'BBC Sports Personality' wa mwaka.
December 31 - Anatangazwa kuwa mchezaji wa muongo wa United(Manchester United Player of the Decade).
2010: February - Anashinda League Cup kufuatia United kuichapa Aston Villa bao 2-1 katika fainali.
2011: January 17 - Anakamilisha mchezo wake wa 600 wa ligi akiichezea United, dhidi ya Tottenham ndani ya uwanja wa White Hart Lane.
2012: February - Anakamilisha mchezo wake wa 900 akiwa na United, akifunga goli la dakika ya mwisho katika ushindi wa magoli 2-1 wakiwa ugenini dhidi ya Norwich.
June - Anatajwa kuwa mchezaji mwenye umri mkubwa kuichezea Great Britain katika michezo ya Olympic.
August - Team GB inatolewa nje ya michezo ya Olympics katika robo fainali ikifungwa na Korea Kusini kwa penati.
2013: February 10 - anafunga goli la kwanza katika mchezo wa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Everton, akiendeleza rekodi yake ya kufunga katika kila msimu katika kazi yake ya kusukuma gozi ambapo katika mchezo wa marudiano timu hizo hazikufungana.
March 5 - Anakamilisha mchezo wake 1,000 katika mchezo wa kiushindani katika mchezo wa ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid katika hatua ya mtoano ya timu 16 bora.
May - Anakuwa ni mmoja wa wachezaji wa United wanaochukua taji la 'Premier League' ikiwa ni kwa mara ya 13.
July 4 - United inamthibitisha Giggs kuwa kocha mchezaji kuanzia msimu wa 2013-14 chini ya meneja mpya David Moyes.
2014: April 22 - Kufuatia kufukuzwa kwa Moyes, Giggs anatangazwa kuwa meneja wa muda.
May 19 - Anatanga kustaafu kama mchezaji kufuatia tangazo rasmi la United kumtangaza Louis van Gaal kuwa meneja mpya.

No comments:
Post a Comment