KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, May 11, 2014

Ujenzi wa viwanja kombe la dunia nchini Brazil 2014, fundi mwingine afariki dunia

The Arena da Baixada mjini Curitiba, Brazil,  wataandaa michezo ya kombe la dunia mwaka huu(Picture: AP Photo)
Wiki nyingine ambayo maisha ya mtu yanapotea.Vifo hivi ni vingi kiasi kuwagharimu wenyeji wa fainali ya kombe la dunia Brazil.

Bila shaka kifo hiki kinatokea si tu katika macho ya serikali ya Brazil bali pia si kwa chama cha soka cha nchi hiyo na shirikisho la soka duniani Fifa.

Muhammad Ali Maciel alikuwa na umri wa miaka 32 akifanya kazi ya kuweka mifumo ya kimtandao wa mawasiliano ndani ya Arena Pantana mjini Cuiaba alipigwa na shoti ya umeme na licha ya jitihada kubwa kufanywa na timu ya madaktari hatimaye alifariki dunia.

Kifo cha Muhammad kinakuwa kifo cha mtu wa nane katika maandalizi ya viwanja kwa ajili ya fainali zijazo za kombe la dunia ambazo zitaanza kupigwa wiki tano zijazo kuanzia sasa.

Kwakweli hizi ni takwimu kubwa na zinaweza kuitia aibu kamati ya maandalizi ya kombe la dunia nchini Brazil 2014, michuano ambayo haitasahaulika kutoka na majanga ya aina hii.

Kutokana na muda uliosalia kuwa mdogo, presha imepanda mno katika kuhakikisha kila kitu kinakamilika kwa wakati, ambapo njia zinazotumika kukamilisha maandalizi zikizongwa na njia nyingi za mkato ambazo bila shaka zitahitaji hatua kubwa za kiusalama kuchukuliwa.

 Inasikitisha sana,kwani viwanja hivyo vinatarajiwa kukusanya watu wengi na wachezaji wengi wakubwa wenye uwezo wa kifedha multi-millionaire kutoka kila kona ya dunia.

Kama mpenda mpira wa miguu bila shaka hili linaumiza sana.

Lakini si wewe tu utakaye umia na hili na kukatishwa tamaa na ongezeko la kupotea kwa maisha ya watu, bali pia kumbuka Brazil taifa kubwa katika soka lenye watu wengi wenye wazimu wa mchezo huo.

Lakini jambo la kushangaza ni pale ambapo maelfu ya raia wa Brazil mara kadhaa walikuwa waliripotiwa kuingia mitaani katika kampeni ya kupinga kuwa waandaaji wa mchezo huo pendwa kote ulimwenguni.

Tatizo lao kubwa ilikuwa ni matumizi makubwa ya fedha kutumika katika maandalizi hayo lakini kama hiyo haitoshi.

Bahati kubwa itakuwa ni katika maandalizi ya michuano hiyo Brazil itaimarisha miundo mbinu yao katika miji mingi ambayo michezo ya fainali hizo itapigwa.
Swali ni je kama pesa zitapatika kuwajengea wale ambao kwa bahati mbaya watakuwa wameondokewa na wapendwa wao?
Dying for the World Cup? Fifa must stop turning a blind eye to Brazil and Qatar
The Mineirao stadium mjini Belo Horizonte nao utatumika kwa michezo ya kombe la dunia(Picture: AP)
Wakati wa-Brazil walipoaanza kupaza sauti zao kupinga taifa lao kuandaa michuano hii mikubwa ya mpira wa miguu duniani ilionekana kutajitokeza mambo ambayo yatakwenda mrama.

Matatizo haya na ukuaji wa idadi ya vifo nchini Brazil inapeleka taswira kwenye maandalizi mengine nchini Qatar mwaka 2022.

Mchezo wa mpira wa miguu huwakutanisha pamoja wapenda michezo katika mchezo unaopendwa kwasababu unaleta kwa pamoja tamaduni na vilevile kombe la dunia siku zote utakuwa ukionekana kwa kipindi chote cha mwezi mzima kama jamboree ambapo watu wataburudika na kila mchezo wa timu shirika.

Kwasasa inaonekana thamani ya maisha ya watu inamezwa na fedha.

No comments:

Post a Comment