Inaaminika kuwa Tottenham huenda wakashangaza wengi kwa kumsajili mlinzi wa kushoto aliye huru wakati wa kiangazai Ashley Cole.
Mlinzi huyo anatarajiwa kuondoka Stamford Bridge baada ya mkataba wake kumalizika mwishini mwa msimu licha ya kwamba bosi wa Chelsea Jose
Mourinho kusema kuwa hadhani kama Cole au John Terry, ambao muda wao unaelekea kumalizika wataondoka.
Na wakati Liverpool wakionekana kuwa katika mpango wa kumpatia mkataba Cole katika kipindi cha wiki kadhaa walionekana Manchester City nao wakionyesha nia huku joto likizidi kuongezeka kwa wakazi wa London ya Kaskazini Tottenham pia wakianza kufikiria kumnyakuwa mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 33 kwa lengo la kuziba nafasi ya Danny Rose aliyeshuka kiwango chake.
Cole amekuwa akihangaika kupata nafasi ya kudumua darajani msimu huu ambako mlinzi wa kulia Cesar Azpilicueta akihamishiwa upande wa kushoto na Mourinho kwa karibu nusu ya kampeni ya msimu huu.
Na kwasasa nafasi ya Cole katika kikosi cha timu ya taifa imekuwa mashakani ambapo mlinzi wa Southampton Luke Shaw ikionekana wazi kuwa atatajwa na kocha wa England sambamba na mlinzi wa Everton Leighton Baines.
No comments:
Post a Comment