Mchezaji mmoja wa timu ya ligi ya soka ya Marekani,
National Footbal League ,Michael Sam amekuwa mchezaji wa kwanza
kutangaza wazi kwamba yeye ni shoga katika mchezo huo.
Sam alikuwa ameteuliwa na timu ya Saint Louis
Rams katika siku ya mwisho ya usakaji wa vipaji katika mchezo huo ulio
maarufu zaidi nchini marekani.
Hatua hiyo ya Michael Sam kutangaza jinsia yake
mnamo mwezi february baada ya kukamilisha masomo yake ya mchezo huo
katika chuo cha Missouri ilipongezwa ,huku rais Obama akiwa miongoni mwa
watu waliotoa pongezi zao.
Baadhi ya wachambuzi wa michezo walikuwa
wamebashiri kwamba baadhi ya timu huenda zikajitenga na umaarufu
unaomzunguka mchezaji huyo.
No comments:
Post a Comment