KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, June 25, 2014

Uchaguzi Simba: Evance Aveva azindua kampeni akisema atarejesha umoja ndani ya klabu hiyo

Mgombea nafasi ya uraisi wa klabu ya Simba Evance Elieza Aveva hii leo ameziundua rasmi kampeni za kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa klabu hiyo ambao umepangwa kufanyika mwishoni mwa juma hili jijini Dar es salaam.
Evance Aveva ambaye anawani nafasi ya uraisi sambmaba na mpinzani wake Andrew Tupa amesema kukubwa ambacho atakipigania endapo atapata ridhaa kutoka kwa wanachama ni kuhakikisha umoja unarejea ndani ya Simba na kasha masuala mengine ya kimaendeleo yatafuata.
Amesema kwa sasa klabu bya Simba imekosa sifa ya kuwa na umoja miongoni mwa wanachama hali ambayo imekua chanzo cha baadhi ya mambo kuharibika kuanzia nje hadi ndani ya uwanja na kupelekea timu yao kufanya vibaya kwa miaka mitatu mfululizo.
 Hata hivyo Aveva akasisitiza kwa kuweka mkazo suala la klabu ya simba kurejesha hadhi yake ya kucheza soka kama ilivyokua miaka ya nyuma na kufikia hadhi ya kutamba katika michuano ya kimataifa.
Amesema siri ya kurejewa kwa mafanikio hayo ni kutengeneza kikosi cha wachezaji kwa kuangilia mpango wa muda mrefu na mfupi.
  Katika hatua nyingine aliyekuwa mwenyekiti wa simba kabla ya uongozi unaomaliza muda wake kuingia madarakani mwaka 2010, Hassan Dalali ambae yupo bega kwa bega na Evance Aveva amewataka wagombea nafasi mbali mbali wa klabu hiyo kuacha kasumba ya kuchafuana katika kipindi hiki cha kampeni na badala yake watumie nafasi ya kuomba kura kistaarabu.
  Wakati huo huo Gefrey Nyange Kaburu anaewani nafasi ya makamu wa raisi wa klabu ya Simba nae amezindua kameni zake rasmi hii leo ambapoa ameahidi kuendeleza mazuri ndani ya klabu hiyo endapo atapata nafasi ya kuchaguliwa na wanachama siku ya jumapili.
  Nae swed Nkwabi ambae anawani nafasi ya makamu wa raisi wa klabu ay Simba amezindua kampeni zake hii leo mitaa ya kariakoo jijini Dar es salaam, ambapo kubwa aliloliahidi ni kurejesha umoja na mshikamano ndani ya klabu ya Simba.