KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, June 25, 2014

SPOTANZA yasisitiza juu ya suala la mikataba ya wachezaji

Mwenyekiti wa SPOTANZA Abeid Kasabalala
Chama cha wachezaji wa mpira wa Miguu nchini SPUTANZA kimeendelea kusisitiza suala la kuingilia kati mikataba ya wachezaji ambao ni wanachama wa chama hicho na klabu watakazosajiliwa kwa lengo la kulinda maslahi yao ya sasa pamoja baadae.
Katibu msaidizi wa SPUTANZA Abeid Kasabalala amesema mwishoini mwa mwezi May walitoa tamko la kuwa makini katika mikataba ya wachezaji hususan katika kipindi hikia mbacho wachezaji wengi wamekua wakifanya makubaliano na klabu wanazokubali kuzitumikia kwa ajili ya msimu mpya wa ligi.
Mwenyekiti wa klabu ya Simba Ismail Aden Rage aking'aka juu ya usajili wa mlinzi Kelvin Yondan aliyetokea Simba na kujiunga na Yanga usajili uliokuwa na utata
Amesema kwa kipindi kirefu wamekua kimya na wameshuhudia namna wachezaji wanavyo dhulumiwa haki zao stahiki, hivyo wameamua kuingia kikamilifu katika harakati za kuhakikisha kila mchezaji anajua haki zake kimkataba.
 
 Katika hatua nyingine Abeid Kasabalala akawataka viongozi wa klabu za ligi kuu pamoja na ligi daraja la kwanza kuwa na utaratibu mzuri wa kuendesha klabu zao, kwa lengo la kuwajengea mazingira mazuri wachezaji wanaowaandaa kwa ajili ya msimu mpya wa ligi.
Kasabalala ametoa rai hiyo kwa viongozi wa klabu kupitia klabu ya Simba ambayo kwa sasa ipo katika harakati za kufanya uchaguzi pamoja na usajili wa wachezaji.