KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, June 26, 2014

ADHABU YA SUAREZ NI ZAIDI YA KAWAIDA HARUHUSIWI HATA KUIHAMA LIVERPOOL

Under the cosh: Luis Suarez, pictured in the hours up to his ban, heads to Uruguay training
Luis Suarez, katika picha saa kadhaa kabla ya kutangaziwa kifungo chake akielekea katika mazoezi ya timu ya taifa ya Uruguay

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uruguay Luis Suarez amefungiwa mechi tisa na shirikisho la kandanda duniani Fifa baada ya kupatikana na hatia ya kumng'ta mlinzi wa timu ya Italia Giorgio Chiellini kwenye mechi yao ya kombe la dunia nchni Brazil.
Suarez pia amefungiwa kutojihusisha na shughuli yoyote ya kandanda kwa miezi minne na kutozwa faini ya dola elfu mia moja.

 
Kutokana na adhabu hiyo Suarez sasa hatashiriki tena kwenye mechi zilizosalia za kombe la dunia.
Kutokana na adhabu hiyo iliyochukuliwa na kamati ya nidhamu ya Fifa Suarez sasa hatashiriki kwenye mechi ya raundi ya pili kati ya Uruguay na Columbia Juni tarehe 28.
Adhabu hiyo pia inamaanisha Suarez hatashiriki kwenye mechi za Uruguay zijazo za kombe la dunia endapo timu itazidi kusonga mbele na zile zijazo za kufuzu kwa mashindano ya kombe la dunia.
Kamati hiyo ya nidhamu ya Fifa imesema Suarez hatakiwi kuingia kwenye uwanja wowote Uruguay inapocheza wakati wa adhabu hiyo ya kutocheza mechi tisa za kimataifa.
Mwenyekiti wa kamati ya nidhamu ya Fifa Claudio Sulser amesema:"Hatuwezi kuruhusu tabia duni kama hii uwanjani hasa wakati wa kombe la dunia kwani mamillioni ya mashabiki kote duniani wanafuatilia mashindano haya. Kamati ya Fifa imetilia maanani kila kitu kwenye kitendo hicho kabla ya uamuzi huo.Tayari tumemjulisha mchezaji huyo na shirikisho la kandanda la Uruguay.''
Mashabiki wengi duniani wamemshutumu vikali Suarez kwa kumng'ata mchezaji huyo wa Italia kwani hii ni mara ya tatu anapatikana na hatia hiyo.
Lakini mashabiki, waandishi wa habari wa Uruguay na shirikisho la kandanda nchini humo wamemtetea mchezaji wao,wakisema hizo ni njama za kumuangamiza Suarez ambaye huichezea Liverpool ya England


Head down: It is the third time Suarez has been banned for biting an opposition player
Suarez akiinamisha kichwa chini na hii ni mara ya tatu anakumbana na adhabu ya kumng'ata mchezaji wa timu pinzaniSecurity: Uruguay's team hotel in Natal has been surrounded by armed guards in response to the incident
Hoteli iliyoko kambi ya Uruguay mjini Natal ilizingirwa na wanajeshi wataki wa tangazo la kufungiwa na FIFADecision maker: Claudio Sulser said the incident 'could not be tolerated on any football pitch'
Mwenyekiti wa kamati ya nidhamu ya Fifa Claudio Sulser akifungua vifungu katika kitabu cha kanuni na maadili cha 'Fair Play'


Chomping at the bit: Luis Suarez appears bites Giorgio Chiellini during Uruguay's 1-0 win
 Luis Suarez akionekana dhahiri akimng'ata Giorgio Chiellini wakati wa mchezo wa ushindi wa Uruguay wa bao 1-0.

LIVERPOOL GAMES SUAREZ MISSES

Aug 16: Liverpool v Southampton
Aug 23: Manchester City v Liverpool
Aug 30: Tottenham Hotspur v Liverpool
Sep 13: Liverpool v Aston Villa
Sep 16: Champions League matchday 1
Sep 20: West Ham United v Liverpool
Sep 27: Liverpool v Everton
Sep 30: Champions League matchday 2
Oct 4: Liverpool v West Bromwich Albion
Oct 18: Queens Park Rangers v Liverpool
Oct 21: Champions League matchday 3
Oct 25: Liverpool v Hull City
Rais wa chama cha soka cha Uruguay Wilmar Valdez amethibtisha tangazo la adhabu hiyo dhidi ya Luis Suarez.
Wadhamini wa mchezaji huyo kampuni ya Adidas wameitisha kikao cha dharura kufuatia tangazo hilo.
Uruguay wanahakikisha kuwa watawasilisha rufaa yao juu ya adhabu hiyo lakini ni wazi kuwa Suarez ataukosa mchezo wa kesho wa hatua ya mtoano ya 16 dhidi ya Columbia katika dimba la Maracana.

Kwa mujibu wa hukumu hiyo ya kisoka kwa Suarez ni kuwa hataruhusiwa kuingia katika uwanja wowote wa mpira ambao timu ya taifa ya Uruguay itakapo kuwa ikicheza katika kipindi chote cha adhabu hiyo wala kujihusisha kwa vyovyote vile na mambo ya kisoka.

Hiyo pia ina mzuia Suarez kufanya uhamisho kutoka katika klabu yake ya Liverpool mpaka mwishoni mwa mwezi October.

MORE THAN A FULL SEASON...

Luis Suarez's bans for various bites now total 39 games.
Ajax – 7 matches for bite on PSV’s Otman Bakkal
(Ajax score first)
Nov 28, 2010: VVV Venlo (a) 2-0
Dec 4, 2010: NEC Nijmegen (h) 1-1
Dec 12, 2010: Vitesse Arnhem (a) 1-0
Jan 19, 2010: Feyenoord (h) 2-0
Jan 23, 2011: FC Utrecht (a) 0-3
Jan 30, 2011: NAC Breda (a) 3-0
4 Feb, 2011: De Graafschap (h) 2-0

Liverpool – 10 matches for bite on Chelsea’s Branislav Ivanovic
(Liverpool score first)
Apr 27, 2013: Newcastle (a) 6-0
May 5, 2013: Everton (h) 0-0
May 12, 2013: Fulham (a) 3-1
May 19, 2013: QPR (h) 1-0
Aug 17, 2013: Stoke (h) 1-0
Aug 24, 2013: Aston Villa (a) 1-0
Aug 27, 2013: Notts County (h) 4-2 – League Cup
Sep 1, 2013: Man Utd (h) 1-0
Sep 16, 2013: Swansea (a) 2-2
Sep 21, 2013: Southampton (h) 0-1

Liverpool – Four months (13 matches) for bite on Italy’s Giorgio Chiellini
Aug 16: Liverpool v Southampton
Aug 23: Manchester City v Liverpool
Aug 30: Tottenham Hotspur v Liverpool
Sep 13: Liverpool v Aston Villa
Sep 16: Champions League matchday 1
Sep 20: West Ham United v Liverpool
Sep 23: Capital One Cup Third Round
Sep 27: Liverpool v Everton
Sep 30: Champions League matchday 2
Oct 4: Liverpool v West Bromwich Albion
Oct 18: Queens Park Rangers v Liverpool
Oct 21: Champions League matchday 3
Oct 25: Liverpool v Hull City