KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, June 12, 2014

Arsenal kulipwa pauni milioni 5 na Chelsea kufuatia mauzo ya Fabregas

Jose Mourinho anakaribia kumpata Fabregas (Picture: EPA)
Chelsea italazimika kuilipa Arsenal pauni milioni 5 endapo watafanikiwa kukamilisha mpango wa kumsajili kiungo wa Barcelona  Cesc Fabregas.
Chelsea wanaonekana kukamilisha usajili wa kiungo huyo baada ya mazungumzo ya wiki hii ambapo habari kutoka katika vyombo vya habari nchini Hispania zinasema tangazo rasmi la kutua darajani kwa kiungo wa zamani wa Arsenal zitatolewa siku chache zijazo.
Arsenal imepiga chini wazo la kutaka kumrejesha kungo huyo ambaye alikuwa nahodha wao kabla ya kuelekea Barcelona lakini sharti moja la makubaliono ya uhamisho wake kuelekea Barca lilikuwa ni endapo atauzwa watafaidiaka na kiasi fulani cha fedha kutoka  Nou Camp.

Chelsea's Portuguese manager Jose Mourinho reacts during the FA Cup 5th round soccer match match between Manchester City and Chelsea FC in Manchester. (Picture: EPA)
Jose Mourinho

Kwa mujibu wa gazeti la Telegraph, ni kuwa kiasi cha pauni milioni hivi zitawasilishwa kwa washika mitutu kitu ambacho kimsingi kimekubaliwa na Chelsea.
Fabregas anarejea Premier League ikiwa ni kipaumbele chake baada ya wiki mbili zilizo pita kuelezwa kuwa anaweza kuihama Barcelona.