KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, June 6, 2014

WORLD CUP: ROBIN VAN PERSIE ANASEMA YUKO FITI KWA ASILIMIA 100

Robin van Persie na kikosi kizima cha Uholanzi wakiwasili Rio
Nahodha wa Uholanzi Robin van Persie amesema kuwa yuko fiti kwa asilimia mia moja kwa ajili ya fainali za kombe la dunia.
Nahodha huyo amesema hayo wakati kikosi cha Uholanzi kikiwasilia katika jiji la Rio de Janeiro hii leo.
Mshambuliaji huyo wa Manchester United alitolewa uwanjani wakati wa mapumziko katika mchezo wao wa mwisho wa maandalizi ya fainali hizo dhidi ya Wales mjini Amsterdam Jumatano kutokana na matatizo ya msuli lakini amesisitiza kuwa ilikuwa ni tahadhari tu baada ya kujisikia kutokuwa katika hali nzuri.
Van Persie ameongeza kwa kusema merejea kuwa katika nzuri baada ya kuwa nje kwa takribani miezi miwili kuelekea mwishoni mwa michezo ya ligi kuu ya Premier League season.
Arjen Robben akisaini autographs jijini Rio baada ya kuwasili hii leo
Uholanzi itakabiliana na Chile na Australia katika kundi la B katika fainali hizo.

No comments:

Post a Comment