Wayne
Rooney amekuwa akiongoza vichwa vya habari baada ya kuonyesha soka bovu katika mchezo dhidi ya Peru,
kiasi kupelekea kocha wa England Roy Hodgson kumchezesha pembeni katika mchezo dhidi ya Ecuador, huku mjadala mkubwa ukiibuka juu ya nani atakaye anza katika kikosi cha kwanza baina yake na Daniel
Sturridge hususani katika mchezo dhidi ya Italia katika dimba la Manaus?
Ingawaje Rooney alikuwa kwenye kiwango cha juu, lakini sitamchezesha katika nafasi ya mshambuliaji wa pili.
Ni kazi ya usaidizi kwa Sturridge lakini ni muhimu sana inajumuisha kazi ya kukabiliana na Andrea Pirlo.
Rooney
alipewa jukumu hilo katika mchezo wa robo fainali ya Euro 2012 sambamba na Andy
Carroll, alishindwa kukabiliana na mkongwe huyo mchezeshaji.
Watu wanazungumzia juu ya kazi nzuri ya Rooney anapokuwa mbele lakini mimi siendani na nadharia hiyo.
Ni kweli anaweza, amefanya hivyo katika klabu yake na timu ya taifa kwa miaka kadhaa, lakini nafikiri kuwa Rooney alikuwa bora zaidi katika msimu wa 2009-10.
Ni kweli anaweza, amefanya hivyo katika klabu yake na timu ya taifa kwa miaka kadhaa, lakini nafikiri kuwa Rooney alikuwa bora zaidi katika msimu wa 2009-10.
Wakati huo alifunga magoli 34 na kushinda tuzo ya mchezaji bora wa PFA.
Usisahau Sir Alex Ferguson alimtumia Danny Welbeck kama mshambuliaji wa pili badala ya Rooney, kumzuia Xabi Alonso katika mchezo dhidi ya Real Madrid katika mchezo wa ligi ya mabingwa Ulaya msimu kabla ya huu uliopita. Alonso ni Pirlo wa Madrid.
Sio suala la Rooney kukosa uwezo, ukweli ni kwamba nafikiri anafanya kazi ngumu kwa wakati fulani na wala simshushi Rooney isipokuwa ni kwasababu za kiufundi ndio maana kiungo anahitajika zaidi kupambana na Pirlo.
Mambo kaka Rejesha Virus keshaondoka mbona kwangu naziona Updates za story zako !
ReplyDelete