KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, June 9, 2014

KIMATAIFA: FIFA YAIPIGA MARUFUKU ARGENTINA, KIKOSI CHA ENGLAND CHAMBERLAIN NJE.......


FIFA YAIPIGA MARUFUKU ARGENTINA NA  JUMBE ZAO ZA  KISIASA
 FIFA imethibtisha kuwa itachunguza tukio la kikosi cha Argentina kuonyeshwa uwanjani kitambaa kilichukuwa na ujumbe wa kisiasa mwishino mwa juma.
Wachezaji wa Argentina walifungua bango lilikuwa na maneno 'Las Malvinas Son Argentinas' (The Falklands are Argentine) na hiyo ilikuwa ni kabla ya mchezo dhidi ya Slovenia Jumamosi usiku.
Timu hiyo iliwahi kuonyesha maneno hayo kwenye kitambaa cha matangazo huku tukielekea kwenye fainali za kombe la dunia tukio hilo limeanza kuamsha hisia mpya.
FIFA, ambayo hairuhusu jumbe za mambo ya kisiasa wakati wa michezo imethibitisha hilo kupitia Sky Sports News kuwa itapiatia upya tukio hilo ambalo huenda likaibua adhabu kwa Argentina.
Argentina iliwahi kuvamia visiwa vya Falkland mwaka 1982, lakini majeshi ya Uingereza yalizima uvamizi huo katika kipindi cha muda mfupi licha ya mauaji makubwa kutokea.
Argentina ilipoteza wanajeshi wake 649 wakati wa vita hiyo huku Uingereza ikipoteza wanajeshi 255. Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na mazungumzo na kura za maoni endapo kuna watu wa Falklands ambao wangetaka kisiwa chao kusalia Uingereza ambapo watu 1513 wamesema ndio na watatu wakisema hapa.
Utawala wa visiwa hivyo umesalia kuwa gumzo nchini Argentina ambapo watu wengi wanataka warejee kuwa chini ya udhibiti wa Argentine.

ENGLAND YAANZA MAZOEZI BILA CHAMBERLAIN
Kikosi cha timu ya taifa ya England tayari kimewasili katika eneo lao la kuanza maandalizi katika jiji la Rio de Janeiro yakiwa ni maandalizi ya full training kuelekea mchezo wao wa kwanza wa kundi D dhidi ya Italia Jumamosi ambayo itakuwa ni jioni kwa saa za Brazil lakini kwa Afrika mashariki itakuwa ni usiku mwingi.
Manager Roy Hodgson ndiye anayetazamwa sasa kufanya maamuzi ya ikosi cha kwanza kwa mchezo huo katika uwanja wa Manaus, ikiwa na pamoja kuangalia uwezekano wa ubora wa afya ya Alex Oxlade-Chamberlain.
Kama ilivyo tazamiwa tangu hapo kabla kabla kiungo huyo wa Arsenal hakufanya mazoezi katika siku hiyo ya leo ya kwanza huku wengine 22 waliosalia wakifanya mazoezi huku Alex akiendelea kuuguza mguu wake kufuatia maumivu aliyoyapata katika mchezo wa kirafiki wa kupasha mwili moto wiki iliyopita mjini Miami dhidi ya Ecuador.
Nafasi yake kikosini imekuwa ikizungumzwa sana na wachambuzi wengi wa mambo ya soka kutokana na umuhimu wake kiasi wengine wakijaribu hata kuonyesha wasiwasi wao juu ya pengo lake.

Mawazo ya wengi wanataka kiungo mwenye umri wa miaka 20 endapo hatakuwa katika nafasi nzuri ya kucheza mpaka siku ya mchezo wa kwanza basi Hodgson atalazimika kumtumia Wayne Rooney ambaye naye nafasi yake inaonekana kuwa katika mashaka kufuatia pendekezo la Hogson kuwa anapendelea kumtumia Daniel Sturridge.
Pendekezo la mwandishi Collins wa Sky Sports anasema Rooney anaweza kucheza vema katika sehemu ya kiungo nyuma ya huku akikazia mawazo yake kwa kusema “leaving Rooney out is unthinkable”
Huenda Hodgoson anafikiria kumtumia Ross Barkley dhidi ya Italia.

AC MILAN YAMFUTA KAZI SEEDORF
Taarifa zilizo arifiwa leo kutoka katika klabu ya AC Milan ni kuwa klabu hiyo imemfuta kazi Clarence Seedorf baada ya kuifindisha klabu hiyo kwa miezi mitano na nafasi yake kuchukuliwa na Filippo Inzaghi as his replacement, the Italian giants confirmed on Monday.
Seedorf alichukua nafasi hiyo San Siro mwezi Januari kufuatia kuondolewa kwa Massimiliano Allegri huku akiwa bado katika mkataba wa miaka miwili.
Seedorf mwenye umri wa miaka 38 ambaye hapo kabla hakuwa na uzoefu wa kufundisha kucheza mpira alipoteza mapenzi kwa Milan kufuatia kuendeleza matokeo mabovu na kiwango kisicho furahisha.
Taarifa ya klabu imesema
"AC Milan inatangaza kumsimamisha kazi kocha Clarence Seedorf na nafasi hiyo ataendelea nayo Filippo Inzaghi mpaka June 30, 2016."
Chini ya Seedorf, Milan imeshinda michezo saba katika michezo tisa ya kumalizia msimu lakini klabu hiyo ilimaliza katika nafssi ya nane katika msimamo wa ligi iliyopita nchini Italia Serie A na kushindwa kupata nafasi ya ushiriki wa ligi za Ulaya kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 16.
Inzaghi hivi karibuni alikaririwa akisema kuwa yuko tayari kuaanza kuifundisha timu ya wakubwa.
Inzaghi sasa ana umri wa miaka 40 akiichezea Milan misimu 11 ambapo alishinda mataji mawili ya Serie A na kushinda vilabu bingwa Ulaya mara mbili kabla ya kustaafu 2012.
Inzaghi, ambaye pia ni mfungaji mwenye rekodi ya mabao mengi mengi katika mashindano barani Ulaya ya magoli 43 amekuwa akiifundisha timu ya vijana ya Milan kwa misimu miwili iliyopita.
Performances yake katika timu ya watoto imeonekana kumkuna mmiliki wa klabu hiyo Silvio Berlusconi.
Wiki iliyopita alimuuliza Inzaghi kama anaweza kumrithi Seedorf, Berlusconi kisha akarejea na majibu
"I see Inzaghi very determined.
"He is hungry for victories.
"He is consistent with what we want Milan to be, that is a team that goes out to win and wins convincingly.
"A team that wins fair and that makes the fans happy with their performances."

Inabakia kuwa ni maswali nini ambacho Inzaghi atakuwa nacho wakati wa msimu ujao.
Kuna tetesi kuwa kiungo Rocaldo Kaka raia wa Brazil ataihama klabu hiyo ambapo huenda akaelekea nchini Marekani kucheza katika ligi kuu ya huko Major League Soccer.
Milan maarufu kama Rossoneri imemsajili mlinzi wa Paris St Germain Alex na pia wanazamiwa kumchukua winga WA klabu hiyo Jeremy Menez .
Bila shaka huenda akasalia na nyota Mattia De Sciglio, Ignazio Abate na Mario Balotelli wachezaji hao wa Milan kwasasa wanaunda kikosi cha kocha Cesare Prandelli cha Italia.
Shida kwa Inzaghi itakuwa ni kumkosa nahodha Riccardo Montolivo katika kuanza kwake majukumu kufuatia kiungo huyo mzoefu kupata majeraha hivi karibuni katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Jamhuri ya Ireland.

 MGOMO MWINGINE TENA KUELEKEA KOMBE LA DUNIA
Wafanyikazi wa usafiri wa mjini Sao Paulo wamepiga kura kuidhinisha mgomo wao uendelee kwa mda usiojulikana licha ya uamuzi wa mahakama ya leba nchini humo, iliyokuwa imewaamuru wafanyikazi hao kurudi kazini mara moja.
Koti ilikuwa imesema wakuu katika vyama vya wafanyikazi hao wa usafiri wa mjini Metro, walikuwa wametumia mamlaka yao vibaya kwa kuanzisha mgomo tangu alhamisi iliyopita.
Huku nusu ya vituo vya usafiri vikiwa tayari vimefungwa, msongamano wa magari umezidi kuizonga Sao Paulo.
Mgomo wa usafiri wazua hofu ya usafiri Brazil

Sasa wasiwasi unaongezeka, wa Je hali ikiendelea hivyo itakuaje hapo alhamisi wakati jiji hilo ndilo linafungua dimba hilo?
Wafanyikazi hao wanadai nyongeza ya mshahara ya asilimia 12 ilhali serkali imesema itamudu nyongeza ya takrban asilimia 9.

 Hatimaye Cameroon waelekea Brazil
Cameroon sasa wameenda Brazil baada ya mzozo kuhusu marupurupu yao kutatuliwa.
Wachezaji hao , almaarufu 'Indomitable Lions' walikuwa wamesusia kuingia ndegeni hadi marupurupu yao yaongezwe.
Akiwemo nyota wao mshambuliaji wa Chelsea, Samuel Eto'o, walikuwa wamegoma kuingia ndegeni hapo Jumapili asubuhi hivyo safari ikachelewa kwa zaidi ya saa 12.
Wachezaji hao walikuwa wakilalamikia kiwango cha fedha £61,000 ambazo walikuwa wamepangiwa kupewa wakisema hazingetosha.
Haijabainika vyema ni idadi gani walichoongezewa ndio wakakubali safari.
Hata hivyo rais wa shirikisho la soka la Cameroon Bw.Joseph Owona amesema 'baada ya kuweka kila kitu wazi ,mzozo huo umetatuliwa na sasa hamna tatizo'.
Tatizo lililopo sasa kwa masimba hao ni kupata mkakati madhubuti wa kukabiliana vilivyo na timu za kundi lao A ambamo wamo miamba ya soka wenyeji Brazil, Croatia na Mexico.

No comments:

Post a Comment