KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, June 6, 2014

GEBO PETER KUZIKWA MKOANI MOROGORO

Mshambuliaji wa zamani nyota wa Sigara, Gebo Peter 
atazikwa kesho mkoani Morogoro.

Msiba wa Gebo aliyefariki leo alfajiri kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili uko Vingunguti Sahara jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa marehebu, Spear Mbwembwe, mwili wa marehebu utasafirishwa kesho alfajiri kwenda Morogoro.

Gebo amefariki baada ya kufanyiwa upasuaji wa henia katika hospitali ya Mwananyamala siku chache zilizopita.

Lakini baadaye akahamishiwa Muhimbili ambako kuanzia juzi hali yake ilizidi kuwa mbaya hadi alipohamishiwa Chumba cha Watu Mahututi (ICU) na leo alfajiri mauti yakamkuta.
TFF yatoa rambirambi…

RAMBIRAMBI MSIBA WA GEBO PETER
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha mchezaji wa zamani wa timu ya Simba na Taifa Stars, Gebo Peter kilichotokea usiku wa kuamkia leo (Juni 6 mwaka huu) katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam.
Gebo aliyezaliwa mwaka 1961, pia aliwahi kuchezea timu za Sigara ya Dar es Salaam, CDA ya Dodoma na kombaini ya Mkoa wa Dar es Salaam (Mzizima United). Hadi mauti yanamkuta alikuwa akijishughulisha na biashara, kubwa ikiwa ya vifaa vya michezo.
Msiba huo ni mkubwa katika familia ya mpira wa miguu nchini kwani, Gebo enzi za uhai wake alitoa mchango mkubwa akiwa mchezaji na baadaye kiongozi katika timu ya Manyema ya jijini Dar es Salaam.
TFF tunatoa pole kwa familia ya marehemu Gebo Peter, klabu ya Manyema na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.
Msiba upo nyumbani kwao Vingunguti karibu na Kanisa Katoliki ambapo taratibu za mazishi zinaendelea kufanywa na familia.
Marehemu ambaye ameacha mjane na watoto watatu anatarajiwa kuzikwa kesho (Juni 7 mwaka huu) nyumbani kwao Kigurunyembe, mjini Morogoro.
Bwana alitoa, na Bwana ametwaa. Jina lake lihimidiwe. Amina
06 Jun 2014

No comments:

Post a Comment