KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, July 26, 2014

Juventus yatoa mashariti kwa Manchester United kuhusu Vidal

Artudo Vidal hajui wapi mlango wa kutokea ulipo
Manchester United yapewa masharti na klabu ya Juventus kama kweli wanataka kumsajili Arturo Vidal.
Taarifa kutoka nchini Italia zinesema kuwa kibibi kizee cha Turin kimewataka wazee wa ngome kongwe kama kweli wanamtaka mchezaji huyo basi wahakikishe hilo linafanyika kabla ya Agosti 2 ambayo ni siku moja kabla ya kufanya safari yao ya kuelekea barani Asia kuanza maandalizi ya msimu.
Vidal amekuwa akihusishwa na kujiunga na Old Trafford msimu huu wa kiangazi huku Liverpool nao wakiripotiwa kuonyesha nia.
Licha ya nyota huyo wa kimataifa wa Chile mara kadhaa kuripotiwa akisema kuwa hajui nini hatma yake ya baadaye, lakini bado hakuna hakuna ofa maalum iliyotoka kwa ajili yake.
Habari kutoka gazeti la kitaliaono la Tottosport zimearifu kuwa Juve imeweka mpaka kufikia Jumamosi ijayo kama kutakuwa hakuna ofa maalum mezani, basi mpango wowote wa uhamisho utakao muhusisha Vidal hautafanyika tena.
Inaelezwa kuwa Louis van Gaal yuko tayari kutoa kiasi cha pauni milioni £39 kwa ajili ya kiungo huyo na huku Liverpool nao wakijipanga kuteka mpango huo wa United kwa dau la pauni milioni £42.5