Vahid Halilhodzic amejiuzulu licha ya ombi la Rais Bouteflika asijiuzulu |
Kocha wa Algeria Vahid Halilhodzic amejiuzulu kazi hiyo licha
ya ombi la kibinafsi kutoka kwa rais Abdelaziz Bouteflika akimsihi
asijiuzulu.
Vahid ambaye amekuwa Kocha wa timu ya Algeria
kwa takriban miaka mitatu na hapo awali meneja wa timu ya Ivory Coast,
alikataa ombi hilo akidai kuwa kuna changamoto za kimichuano.
Vahid ambaye ni mzaliwa wa nchi ya Bosnia
aliipeleka Algeria mpaka kufikia hatua ya mtoano ya michuano ya kombe la dunia nchini Brazil kabla ya kutolewa kishujaa na Ujerumani.
Timu yake ilikuwa
imesalia kati ya timu zingine kumi na sita bora katika hatua hiyo ya kombe la dunia.
Timu ya Algeria baada ya kuilaza South Korea
mabao manne kwa mawili, haikufanikiwa kupona katika hatua ya mtoano baada ya kulazwa mabao mawili
kwa moja dhidi ya timu ya Ujerumani.
Hapo awali, katika michezo ya ufunguzi, Algeria ililazwa mabao mawili kwa moja dhidi ya Belgium,
na kutoka sare ya bao moja kwa moja dhidi ya Urusi na kufuzu kwenda
raundi ya pili.
No comments:
Post a Comment