KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, July 6, 2014

Vita ya usajili wa akiangazi: Mfaransa Moussa Sissoko anaripotiwa kutakiwa na Liverpool na Monaco

Mfaransa Moussa Sissoko anaripotiwa kutakiwa na Liverpool na Monaco
Liverpool imeripotiwa kumtaka kiungo wa Newcastle Moussa Sissoko kwa lengo la kutaka kuimarisha eneo lake la kiungo msimu ujao.
Wekundu hao tayari wamesha onyesha dhamira ya kweli ya kutaka kufanya kweli msimu ujao kwa kuwasajili Rickie Lambert na Adam Lallana wote kutoka katika klabu ya Southampton na sasa wanafikiria kunasa saini ya Sissoko mwenye umri wa miaka 24 hizi zikiwa ni taarifa zilizoripotiwa na gazeti la kifaransa la L’Equipe.
Taarifa zinadai kuwa Monaco nao wanataka huduma ya kiungo huyo wakati huu ambao nao wanajipanga kwa ajili ya ligi ya mabingwa Ulaya kwa mara ya kwanza tangu miaka kumi kupita.
Sissoko alijiunga St James’ Park kwa pauni milioni £1.8 akitokea Toulouse Januari 2013, na bado anaendelea na mkataba wa miaka mitano na klabu hiyo ya Newcastle.