Bodi ya ligi kuu nchini Tanzania imesema kuwa ina orodha ndefu ya waamuzi waliochezesha ligi mwaka jana ambao kimsingi hawatatumika msimu mpya wa ligi 2014/15.
Akiongea na mtandao wa Rockersports mtendaji mkuu wa bodi hiyo Silas Mwakibinga amesema ni kutokana na makosa mbalimbali ya kutafsiri sheria aidha kwa bahati mbati au kwa makusudi Bodi yake imeonelea ni vema kuwaengua baadhi ya waamuzi walionekana na makosa mbalimbali msimu uliopita.
pamoja walipitia ripoti mbalimbali za michezo ya msimu uliopita na kujiridhisaha juu ya matatizo ya usimamiaji wa waamuzi wa ligi msimu uliopitana kwamba maamuzi hayo si ya kumkomoa mtu kwani ripoti hizo zipo ofisini kwake.
Hata hivyo Mwakibinga aligoma katakata kuwataja waamuzi waliopigwa chini na Bodi yake kwa kushirikiana na kamati ya ligi kutokana na sababu za kimaadili huku akiahidi muda ukifika waamuzi hao wataanikwa hadharani.
Aidha amesema kuna baadhi ya michezo wamelazimika kupitia upya mikanda ya video kuangalia matukio ya maamuzi ya wamuzi viwanjani.
Ligi kuu ya Soka nchini msumu mpya 2014/15 inatarajia kuanza Septemba 20 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment