KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, July 11, 2014

Ligi ya soka Tanzania Bara msimu mpya 2014/15 kuchezwa usiku, Uwanja wa Azam Complex watengeneza historia nyingine mpya.


Muonekano wa nje wa uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi
Uwanja wa Azam Complex uliko Chamazi jijini Dar es Salaam unakuwa uwanja wa kwanza kwa upande wa Tanzania Bara kutumika kwa michezo ya ligi kuu ya soka nyakati za usiku.

Akiongea na mtandao huu wa Rockersports, mtendaji mkuu wa bodi ya ligi Silas Mwakibinga amesema kuwa uwanja huo kwasasa unafungwa taa maalumu za kuruhusu mwanga wa kutosha wakati mchezo huku lengo kuu la matumizi ya uwanja huo usiku ikiwa ni kuifanya ratiba ya ligi kuu kwenda na wakati na kumalizika kwa wakati.

Mwakibinga amesema ratiba ya ligi hiyo msimu huu imezingatia mambo mbalimbali kwa lengo la kuifanya kuwa rafiki zaidi akitolea mfano wa kuipishanisha na ratiba ya michezo ya ligi kubwa barani Ulaya ambayo michezo yake mingi mikubwa ilikuwa ikifungana na michezo yenye mvuto kwa hapa nchini na hivyo kupunguza watazamaji wa uwanjani ambao wanafafuatilia ligi za Ulaya na kuathiri mapato ya milangoni.
Uwanja utatumika kwa michezo ya ligi ya ligi kuu nyakati usiku
Amesema kwa kuzingati hayo na mengine yanayofanana na hayo Bodi yake imeonelea ni vema kufanya mazungumzo na uongozi wa Azam fc ili kuona kama kuna uwezekanao wa kuruhusu michezo mingine ya ligi hiyo kupigwa usiku kwenye uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi jambo ambalo kimsingi limekubalika na sasa mchakato wa uwekaji taa maalumu za viwanjani unaendelea.

Hii inakuwa ni historia kwa ligi kuu ya soka ya Tanzania bara kuchezwa usiku kwa mara ya kwanza tofauti na Zanziba ambako uwanja wa Amani umekuwa ukitumika kwa michezo yake ya ligi kupigwa nyakati hizo.

Kumbuka kuwa uwanja huo umeshatengeneza historia ya kwanza kuwa uwanja wa kwanza unaomilikiwa na klabu nchini Tanzania kuruhusiwa na shirikisho la soka barani Afrika CAF kutumika kwa michezo ya kimataifa ya ngazi za vilabu.
Hiyo ilifuatia  jitihada za uongozi wa klabu ya Azam fc ambao ndio klabu bingwa nchini Tanzania kuomba CAF kuwaruhusu michezo yao ya  klabu bingwa Afrika kufanyika uwanjani hapo. 

Kumbuka Ligi kuu ya Soka Tanzania Bara inatarajia kuanza kutimua vumbi Septemba 20 mwaka kufuatia kusogezwa mbele kutoka Agosti 24 kwasababu zilizo elezwa na TFF za kupisha michezo ya kimataifa ya vilabu na timu ya Taifa.