Endapo jezi hii itavaliwa tayari mpango mzima kwa Barcelona kutengeneza fedha kwa kutengenza jezi hii ya Suarez namba 9 mgongoni
|
Luis Suarez ameondoka Liverpool na kukamilisha mipango ya kujiunga na Barcelona kwa pauni milioni £75.
Liverpool imeshakamilisha mambo ya msingi katika kukamilisha rekodi ya uhamisho ya klabu yao kwa Barcelona kwa muuza mshambuliaji Luis Suarez.
Mazungumzo rasmi yalianza karibu wiki sasa na yaonekana kwenda vizuri tangu kuanza kwake ambapo klabu hiyo ya Katalunya imekubali kuvunja mkataba wa mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uruguay kwa kiasi kinacho aminika kuwa ni pauni milioni £75.
Dole gumba mia mia: Luis Suarez amekamilisha uhamisho wa kujiunga na Barcelona wenye thamani ya pauni milioni £75 akitokea Liverpool
Kifungo: Rufaa ya Luis Suarez ya kupinga adhabu ya kufungiwa kucheza soka kwa miezi minne kwa kumng'ata Giorgio Chiellini imegonga mwamba
Kumekuwepo na muendelezo wa mazungumzo ya makubaliano juu ya namna ya kulipana wakati ambapo Liverpool wakionekana kutaka huduma ya mshambuliaji wa kimataifa wa Chile Alexis Sanchez ambaye tayari ameshakamisha mipango ya kujiunga na Arsenal
No comments:
Post a Comment