|
Sami Khedira is on Arsenal's radar but the Gunners could baulk at the £20m-plus asking price |
Arsenal inajaribu kufuatilia gharama nzima ya kumpata kiungo wa Real Madrid Sami Khedira.
Wakiwa tayari wameshafanikiwa kupata saini ya Alexis Sanchez, Washika mitutu sasa wammegeukia mchezaji mwingine kiungo mzuiaji Khedira.
Khedira, ambaye amesaliwa na miezi 12 katika mkataba wake na Real, amekuwa katika kitabu cha orodha ya wachezaji wa kiungo cha mzee Arsene Wenger.
Klabu hiyo imekuwa ikihitaji kujua itawagharimu kiasi gani kumpata Khedira. Lakini wakati wakionekana kumkodolea macho kiungo huyo, inaonekana kuwa huenda uhamisho huo usifanyikiwe kutokana na tatizo la kifedha .
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27 inaaminika kuwa huenda gharama halisi ya kunasa saini yake ikafikia pauni milioni £20 licha ya kusaliwa na miezi 12 ya mkataba ndani ya Madrid.
Kwa kuongezea hapo Khedira mwenyewe anataka angalau kiasi cha pauni £150,000 kwa wiki na kuwa mchezaji anayelipwa pesa nyingi Arsenal.
Arsenal
inao uwezo wa kifedha kukamilisha uhamisho huo lakini imejipanga na pauni milioni £60 kumnasa Sanchez.
|
Alexis Sanchez |
Sambamba na hilo,
washika mitutu pia wamekubali kulipa pauni milioni 11 kwa mlinzi wa kulia wa Newcastle Mathieu Debuchy. Na wakati Wenger akiwa katika mawindo ya mlinda mlango, mlinzi wa kati na mshambuliaji, uhamisho Khedira itakuwa ni hatua muhimu mbele.
Wenger pia anavutiwa na kiungo wa Bayer Leverkusen Lars Bender.
Mtendaji wa washika mitutu tayari amefanya mawasiliano na wakuu wa Leverkusen juu ya Bender.
No comments:
Post a Comment