Liverpool haitarudisha pesa kwa mashabiki wake ambao wamenunua jezi mpya ya klabu hiyo yenye namba na jina la Luis Suarez mgongoni baada ya mshambuliaji huyo kujiunga na Barcelona.
Suarez ameihama Liverpool na kujiunga na Barcelona kwa uhamisho wa pauni milioni 75 zikiwa ni taarifa ambazo zimethibitishwa hii leo.
Shughuli ya utengenezaji jezi ya Suarez sasa inahamia Barcelona |
Kumekuwepo na fununu za karibu majuma kadhaa yaliyopita ambapo sasa hatimaye mshambuliaji huyo ametua Nou Camp.
Kumezuka malalamiko kutoka kwa mashabiki wa kweli wa klabu hiyo ambao wameanza kudai kurudishiwa fedha zao baada ya Liverpool kuwauzia jezi mpya ya Suarez mpaka mapema hii leo.
Liverpool imejibu hilo kwa kusema hakuna pesa itakayorudishwa.
No comments:
Post a Comment