KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, July 11, 2014

Ismail Aden Rage akabidhi nyaraka na mali za Simba kwa Rais mpya wa klabu hiyo Aveva


Rais aliyemaliza muda wake Simba Ismail Aden Rage akabidhi nyaraka na mali ya klabu kwa Rais mpya wa klabu hiyo Evance Aveva
Aliyekuwa mwenyekiti wa klabu ya Simba Ismail Aden Rage hii leo amakabidhi ofisi kwa uongozi mpya wa klabu hiyo ambao unaongozwa na Evance Elieza Aveva mara baada ya kukamilika kwa zoezi la uchaguzi mkuu uliofanyika mwishoni mwa mwezi uliopita.
Ismail Aden Rage amefanya makabidhiano hayo ya ofisi kwenye makao makuu ya klabu ya Simba ambapo amekabidhi nyaraka mbalimbali za kiutendaji wa klabu hiyo kongwe hapa nchini.
Hata hivyo rage ameushauri uongozi wa Evance Aveva kufuata taratibu ambazo alizitumia wakati wa uongozi wake wa kipindi cha miaka minne hususana katika suala la vyanzo vya fedha.
Kitu kingine ambacho Rage amekigusia ni kumtaka Rais wa klabu ya Simba Evance Aveva kutatua kwa kutumia busara suala la wanachama wa klabu hiyo waliokwenda mahakani kwa lengo la kuzuia uchaguzi.
Katika hali ya kushangaza Ismail Aden rage akazungumzia na kukabidhi nyaraka zinazoonyesha uhamisho wa mshambuliaji Emmenuel Okwi ambae aliuzwa na klabu ya Simba huko ndhini Tunisia kwenye klabu ya Etue Du Sahel.
Baada ya kukabidhiwa nyaraka za klabu ya simba Rais mpya Evance Aveva alimshukuru Ismail Aden Rage kwa niaba ya kamati yake ya utandaji huku akimtaka kutojiweka mbali mba wao kutokana na kuona bado kuna hitajiko la nguvu zake ndani ya klabu hiyo ya Msimbazi.