KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, March 30, 2013

YANGA NA SIMBA ZAVUNA ALAMA MOJA KILA MOJA HUKU AZAM WAKIVUNA ALAMA 3 MBELE YA RUVU SHOOTING.

 Ikiwa mkoani Morogoro hii leo ikicheza dhidi ya maafande wa polisi vinara wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara Yanga wamelazimishwa sare ya bila kufungana mchezo uliopigwa katika dimba la Jamhuri mkoani humo.

Sare hiyo imeifanya Yanga kuambulia alama moja tu ambayo imewafanya kufisha jumla ya 49 katika msimamo wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara.

Yanga ilielekea katika mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa bao 1-0 iliyoupata kwa Ruvu shooting ya Pwani.
 Yanga sasa imesaliwa na michezo minne ya ligi hiyo kabla ya kufikia tamati huku mchezo dhidi ya watani wao wakubwa katika soka la Tanzania ukitarajiwa kuchezwa mei 18.

Mchezo ujao Yanga itakuwa ikicheza dhidi ya JKT Oljoro Aprili 10 kabla ya kuifuata Mgambo JKT mkoani Tanga siku tatu baadaye.

Itarejea tena Dar es Salaama kukabiliana na Coast Union siku ya May mosi kabla ya kumsubiri mpinzani wake Simba mei 18.
Wenyewe Simba hii leo wamelazimishwa sare ya mabao 2-2 na Toto Afrika ya Mwanza  katika mchezo uliofanyika katika dimba la CCM Kirumbaanya Simba kuongeza alama moja na sasa wakiwa na 35 
 Katika mchezo ujao Simba watakuwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kukabiliana na wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kombe la Shirikisho Azam fc walio katika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi.
Azam hii leo wamevuna alama tatu muhimu mbele ya Ruvu Shooting baada ya kuchomoza na ushindi wa bao 1-0 bao lililofungwa na mshambuliaji hatari Kipre Tchetche  mchezo uliofanyika uwanja wa Mabatini Mlandizi mkoani Pwani.

 Kwa ushindi wa leo wa Azam fc imefikisha jumla ya alama 43 ikiwa ni alama sita nyuma ya vinara Yanga wenye alama 49.

No comments:

Post a Comment