Rafael
Benitez amejitetea juu ya maamuzi yake ya kufanya mabadiliko madlikom kwa
wachezaji saba katika mchezo wa jana ambao Chelsea ilichapwa bao 2-1 na Southampton
wakati huu ambapo wanaelekea katika mchezo wao wa robo fainali ya michuano ya
FA hapo kesho jumatatu dhidi ya Manchester United.
Walinzi wa David
Luiz na Ashley Cole pamoja na kiungo Eden Hazard hawakuwepo katika kikosi
ambacho kiliishuhudia hapo jana Chelsea ikidondoka kutoka katika nafasi ya tatu
mpaka ya nne ya msimamo wa ligi kuu ya soka England.
Amenuliwa bosi
huyo wa muda akisema
"tumefanya
hivyo ili kuelewa kikosi na kukijenga"
"Hatukuwa
na namna nyingine ya kufanya katika baadhi ya nafasi, tulikuwa na wachezaji hao
tuliokuwa nao"
Gary Cahill hakuwepo
katika mchezo huo dhidi ya Southampton kwasababu ya maumivu ya mguu kama
ilivyokuwa kwa Juan Mata ambaye naye alikuwa ni mgonjwa.
Benitez amesema
"lazima
tukabiliane na hali katika kila mchezo ni jambo muhimu sana na tulidhani kwa
kuwatumia wachezaji hao mambo yangekuwa mazuri.
Licha ya
kwamba huo ulikuwa ni mchezo wa tatu mfululizo kwa Chelsea kufungwa ugenini
katika ligi ambao umewapandisha juu Tottenham, bosi huyo mhispania amesisitiza
kuwa kikosi chake kilikuwa vizuri.
MICHEZO MUHIMU KWA CHELSEA
1 April: H v
Man Utd (FA Cup quarter-final replay)
4 April: H v
Rubin Kazan (Europa League quarter-final first leg)
7 April: H v
Sunderland (league)
11 April: A
v Rubin Kazan (Europa League quarter-final second leg)
Martin O'Neill afukuzwa kazi Sunderland
Sunderland iliyo
katika nafasi ya hatari ya kushuka daraja imemfukuza kazi meneja wake Martin
O'Neill kufuatia matokeo mabaya ya michezo mbalimbali ya ligi kuu ya nchini
England.
Paka mweusi
ana alama moja tu juu ya msatari wa kushuka daraja relegation zone ya Premier
League relegation ikiwa pia imesaliwa na michezo saba jana ilipokea kichapo
kingine cha bao 1-0 kutoka kwa Manchester United.
Sunderland haijashinda
katika michezo nane mfululizo ya ligi kuu na katika jumla ya michezo yote hiyo
imeambulia alama tatu.
Taarifa ya
klabu hiyo imesema kuwa maamuzi ya nani atarithi mikoba ya O'Neill's yatafanyika
katika siku chache zijazo.
Paolo Di
Canio mwenye umri wa miaka 44, anatajwa kuwa mrithi wake.
Meneja huyo
wa zamani wa West Ham United aliondoka katika klabu ya League One ya Swindon mwezi
Februari, ambayo ilikuwa ni klabu yake ya kwanza kama meneja.
Pia meneja
wa zamani wa timu ya taifa ya England Steve McClaren, ambaye naye aliondoka
kibaruani FC Twente mwezi February, anahusishwa na kuchukua nafasi hiyo ya
kazi.
Majina mengine
ni pamoja na meneja wa zamamni waklabu za Queens Park Rangers na Manchester
City Mark Hughes na Roberto Di Matteo
ambaye alitwaa taji la mabingwa Ulaya na michuano ya FA akiwa kama meneja wa
muda wa Chelsea msimu uliopita.
Mchezaji wa
zamani wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer, ambaye kwasasa yuko katika
klabu ya nchini Norway ya Molde, pia anahusishwa na kazi hiyo kama ilivyo kwa
bosi wa Brighton, Gus Poyet.
West Ham imenogewa na mkopo wa Andy
Carroll
Meneja wa West
Ham Sam Allardyce ana imani kuwa atambakisha mshambuliaji wake aliye kwa mkopo
katika klabu hiyo yenye maskani yake Upton Park Andy Carroll mpaka msimu ujao.
Mshambuliaji
huyo mwenye umri wa miaka 24 alifunga
magoli mawili –katika mchezo dhidi ya West Brom na taarifa zinasema kuwa
mshambuliaji huyo yuko mbioni kurejea Liverpool wakati wa kiangazi baada ya
msimu mrefu wa mkopo.
Alipoulizwa juu
ya mfungaji huyo wa zamani wa Newcastle kusalia , Allardyce alijibu kuwa siku
zote amekuwa katika kuamini hilo linawezekana.
"tutaangalia
mwishoni mwa msimu na tutaangali namna ya kufanya mazungumzo"
Carroll alijiunga
na Liverpool kwa uhamisho wa rekodi ya klabu hiyo wa pauni milioni 35 mwezi
januari 2011.
Alisajiliwa ili
kuziba pengo la Fernando Torres kufuatia mhispania huyo kuhamia Chelsea kwa uhamisho
wa pauni milioni 50 lakini hata hivyo Carrol alishindwa kufanya vema Anfield na
tangu wakati huo akapoteza hata nafasi yake katika kikosi cha timu ya taifa ya England.
Mshambuliaji
huyo mrefu wa futi sita alitumikia michezo miwili tu Liverpool chini ya meneja Brendan
Rodgers msimu huu kabla ya kujiunga na washika nyundo mwezi August.
David Beckham anafikira kuongeza msimu PSG
David
Beckham ameweka wazi amedhamiria kuongeza muda wake wa kusalia katika klabu ya
Paris St-Germain ya nchini Ufaranza mpaka msimu ujao.
Nahodha huyo
wa zamani wa timu ya taifa ya England baada ya kumaliza makataba wake katika klabu ya Los
Angeles Galax alikuwa na ofa za vilabu kumi na moja kwa mkataba wa miezi mitano
lakini chaguo lake lilikuwa ni PSG.
Amenukuliwa na
Le Parisien akiuliza
"Ni
nani asiyependa kuwepo sehemu kama hii? Ni sehemu ambayo ambayo kila mtu
anataka kuwepo.".
Kocha wa PSG
cCarlo Ancelotti amesema kuwa
"ningependa
kuona David Beckham akiongeza mkataba"
Ndani ya
kipindi alichokuwepo Paris, Beckham amechangia kuivusha PSG ikitinga robo
fainali ya vilabu bingwa Ulaya na sasa ikisubiri mchezo dhidi ya Barcelona na
wakati huo huo PSG ikisalia katika kilele cha msimamo wa ligi kuu nchini
Ufaransa Ligue 1.
Beckham
ametoa kauli hiyo Ijumaa baada ya mchezo dhidi ya mabingwa watetezi wa ligi ya
nchini humo Montpellier ambapo walichomoza na ushindi wa bao 1-0 ambapo
aliingia dakika 18 za mwisho katika mchezo huo.
Anatarajiwa kuwa
msaada mkubwa katika mchezo dhidi ya Barca akitoa mchango kama mchezaji mzoefu.
Liverpool yaibabua Aston villa
Aston Villa imeshindwa
kujiondoa katika eneo la hatari la uwezekano wa kushuka daraja katika ligi ligi
kuu ya chini England ‘Premier League ‘ kufuatia Liverpool ilitokea nyuma kimatokeo
kuibuka na ushindia wa mabao 2-1 mchezo uliofanyika Villa Park.
Kikosi cha Paul
Lambert kilianza kuandika bao la uongozi kufuatia mpira wa Gabriel Agbonlahor
kumkuta Christian Benteke aliyeandika bao hilo.
Liverpool ilisawazisha
muda mfupi baada ya mpira kuanza kati pale ambapo Jordan Henderson alipo uchopu
mpira uliompita mlinda mlango Brad Guzan.
Naye Steven
Gerrard aliandika bao la pili kwa njia ya penati kufuatia Nathan Baker kumuangusha
Luis Suarez katika eneo la hatari.
Mattsson aikimbia kazi ya kufundisha Sierra Leone.
Kocha wa
timu ya taifa ya Sierra Leone Lars Olof Mattsson ameachana na kazi ya
kuifundisha timu ya taifa ya nchi hiyo baada ya miaka miwili ya kuifundisha
timu hiyo lakini hata hivyo kuna habari za kutatanisha juu ya kujiuzulu kwake.
Kocha huyo
mwenye umri wa miaka 58 raia wa Sweden amedai kuwa tayari alikwisha kuwaandikia
barua chama cha soka cha nchi hiyo (SLFA) na nyingine kwenda kwa waziri wa
michezo. Lakini hata hivyo SLFA na wizara wamekanusha kupokea barua ya Mattsson
Msemaji wa SLFA Sorie Ibrahim amenukuliwa
akisema
“kama anataka kujiuzulu kazi alipaswa
kuwasiliana na sisi kwa kuwa ni mwajiri wake na kwenda kwenye vyombo vya habari
vya Sweden”
"Bado
tunachukulia kocha Mattsson kuwa ni kocha wetu nab ado hatuja pokea barua yake.
Tumesikia taarifa hizi kupitia vyombo vya habari vya Sweden”
Mattsson alielezea
matatizo katika timu ya taifa ya Siera Lione Leone Stars ambayo ameiongoza mpaka mwishoni mwa juma ambapo
walifungwa na Tunisia mabao 2-1 mchezo wa kufuzu kombe la dunia, pia ameelezea kuwa
hana mkataba na SLFA.
No comments:
Post a Comment