KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, April 1, 2013

TAMASHA LA PASAKA LAFANA LICHA YA MVUA KUNYESHA SIPHO MAKABANE , ROSE MHANDO WAKOSHA NYOYO ZA MASHABIKI (Source Lenzi ya michezo blog)

Rose Mhando.
Sipho Makabane.
Sipho akitoa burudani huku akisindikizwa na waimbaji wengine wa Tanzania.
Umati ulikuwepo Taifa.
 Kwaya ya Ambassador ya Rwanda wakitumbuiza.
Anastazia Mukabwa akiwa na wacheza shoo wake.
Upendo Kilahiro akitoa burudani
Boniface Mwaitege akiwa amewabeba wacheza shoo wake.
Kama kawaida Rose akishambulia jukwaa.
LICHA ya mvua iliyonyesha kutwa leo jijini Dar es salaam haikuweza kuzuia umati wa watu wa Mungu kuhudhuria tamasha la paska lililofanyika kwenye Uwanja wa Taifa

Tamasha hilo ambalo limeandaliwa na kampuni ya Msama Promotions, Mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Kayanza Pinda ambaye alikuwa amefuatana na mkewe mama Tunu

Awali akizungumza na umati huo Waziri mkuu alimsifu Msama kwa moyo wake wa kujitolea kwa kusaidia watu ambao hawana uwezo japo alichonacho siyo kikubwa.
"Nampongeza sana Msama kwa moyo wake wa kusaidia wengine kwani anasomesha watoto 40 na sasa anafanya matamasha ili kusaidia watu wengine ambao hawana uwezo hivyo na mimi nampa milioni 10", alisema Pinda

Waimbaji waliopanda kutumbuiza waliweza kukonga nyoyo za mashabiki kiasi cha kushangilia bila kukoma. Miongoni waliokonga nyoyo ni Sipho Makabane toka Afrika ya Kusini, Rose Mhando,Ambassodar kwaya toka Rwanda na wengine wengi

No comments:

Post a Comment