KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, April 1, 2013

MMILIKIWA SUNDERLAND ELLIS SHORT AWAKOROGA MASHABIKI WA SUNDERLAND KWA KUMUAJIRI FASHISTI PAOLO DI CANIO TAHARUKI YA KISIASA YAINGIA SUNDERALAND MAKAMU MWENYEKITI AJIUZULU MASHABIKI WAGOMA.

Controversial: Di Canio has never hidden from his fascist views that have caused upset in Sunderland
Gumzo: Di Canio hakuwahi kuficha hisia zake za kifashist ambapo alisababisha hasira Sunderland.
Sunderland imemtangaza Paolo Di Canio kuwa meneja wake atakaye mrithi wa Martin O’Neill aliyefukuzwa kazi Jumamosi.
Di Canio amesafiri kuelekea Sunderland jana na anatarajiwa kukutana na wachezaji wake wapya hii leo na kuanza mafundisho yake ya kwanza baada ya kumalizika kwa mapumziko ya wiki huko Wearside ikiwa ni masaa 24 baada ya kuchukua nafasi ya O’Neill.

Mmiliki wa Sunderland Ellis Short, ambaye alifanya mawasiliano na Di Canio wiki iliyopita alimuondosha kazini O’Neill baada ya Sunderland kufungwa bao 1-0 na Manchester United Jumamosi.
In the driving seat: Paolo Di Canio has been named as the new boss of Premier League side Sunderland
Bosi mpya wa Sunderland Paolo Di Canio.
Heading north? Paulo Di Canio is understood to be in talks with Sunderland over the vacant managers job

MITIHANI YA DI CANIO NDANI SUNDERLAND.

Chelsea vs Sunderland - Sunday, April 7
Newcastle vs Sunderland - Sunday, April 14
Sunderland vs Everton - Saturday, April 20
Aston Villa vs Sunderland - Monday, April 29
Sunderland vs Stoke - Saturday, May 4
Sunderland vs Southampton - Sunday, May 12
Tottenham vs Sunderland - Sunday, May 19

Bottom of the PL
Hata hivyo baada ya kutajwa Di Canio kuwa meneja mpya wa klabu hiyo, kuliibuka hali ya sintofahamu usiku wa jana kufuatia makamu mwenyekiti David Miliband kuandika barua ya kujiuzulu ambapo mashabiki wa klabu hiyi walitishia kufanya vurugu baada ya mmiliki kumtangaza Di Canio kama ndio chaguo la kuchukua nafasi ya umejea.

Di Canio mzaliwa wa Rome mwenye umri wa miaka 44 hakuwahi kuficha hisia zake na kuunga mkono ufashisti ambapo inaarifiwa kuwa huko nyuma aliwahi kuwapigia saluti ya kifashisti mashabiki wa Lazio jambo ambalo limeingia katika mtazamo wa kisiasa kwa mashabiki wa Sunderland ambao wanajivunia juu ya daraja la klabu yao na pia historia ya klabu hiyo ambayo inafuata misingi ya kijamaa.

Kupitia mtandao wake , Miliband amenukuliwa akisema
‘Kwa mtazamo na maelezo ya kisiasa ya meneja mpya,  nadhani ni vema nijiuzulu’

Usiku wa juzi naye Dave Bowman, mwenyekiti wa kundi la mashabiki wa Sunderland ambalo ni tawi la eneo la Manchester, Greater Manchester branch, alisema ameondoka katika nafasi yake na hatarejea katika uwanjani wakati Di Canio aatakapo kuwa kazini.

Bowman ambaye ni mwanachama mkongwe tangu mwaka 1958, anaamini kuwa Short haelewi kwa undani juu ya hisia za baadhi ya mashabiki.


Controversial: Di Canio has never hidden from his fascist views that have caused upset in Sunderland
Disemba 2005, Di Canio alifungiwa kutokucheza mchezo mmoja kufuatia kupiga saluti kuelekea kwa mashabiki wa Lazio.

 Baadaya kupiga saluti kwa kuonyesha hisia zake juu ya ufashisti, Di Canio alijitetea kwa kitendo hicho huku akiviambia vyombo vya habari vya nchini Italia waziwazi kuwa-
 ‘I am a fascist, not a racist.’

Alionyesha kumpongeza na kumuunga mkono fashisti wa na diktekta wa zamani wa Italia Benito Mussolini katika autobiography yake akisema ni mtu very principled, ethical individual’.

Mmiliki wa Sunderland Short bila kujali yote hayo, amekaririwa akisema 
‘Paolo anashauku na changamoto iliyo mbele yake ana hamu na anasukumwa na moyo wa kufanya kazi haraka.

  Mwelekeo wa sasa ni namna ya kupata matokeo mazuri katika michezo saba ya ligi iliyosalia na kuinusuru klabu hiyo na balaa la kushuka daraja na kulinda heshima ya klabu hiyo 
Short anasema anadhani nafasi ya kufanya hivyo ni kubwa hasa baada ya Paolo Di Canio kujiunga nao.
Quit: David Miliband has resigned from his position at Sunderland after the appointment of Di Canio
David Miliband naye ameamua kuachia ngazi katika nafasi yake ya makamu mwenyekiti kufuatia kuajiriwa kwa Di Canio.

Behind you: Martin O'Neill was sacked after Sunderland lost to Manchester City on Saturday
Picha ya mwisho akiwa meneja wa Sunderland baada ya mchezo dhidi ya Manchester United Jumamosi.


sunderland managers

High hopes: O'Neill is unveiled at Stadium of Light in 2011
 O'Neill's wakati anafika Sunderland Disemba 201. 


Bosi huyo wa zamani wa Leicester na Celtic amekuwa kibaruani kwa miezi 15 baada ya kuajiriwa na Short kurithi nafsi ya mtangulizi wake Steve Bruce wiki chache baada ya aliyekuwa mwenyekiti wa klabu hiyi Niall Quinn kuondoka katika klabu hiyo.

Wakati wa utumishi wake O’Neill aliwasajili Steven Fletcher na Adam Johnson kwa pauni milioni £23 wakati wa kiangazi.
Had enough: Ellis Short made the decision to sack O'Neill

Huyu ndiye mmiliki wa Sunderland Ellis Short analiyefanya yake kumfukuza O'Neill na kumuajiri fashisti Di Canio.

No comments:

Post a Comment