Julio Cesar: Inter ndiyo mpinzani
pekee wa Juventus kuwania Scudettol.
Julio Cesar anaamini
kuwa Inter Milan ndiyo mpinzani pekee wa Juventus katika mbio za kusaka taji la
ligi kuu ya nchini Italia ‘Scudetto’ msimu huu wakati wakielekea katika mchezo
mkubwa maarufu kama ‘Derby d'Italia’ usiku huu.
Nerazzurri kwasasa
wako katika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu ya nchini Italia Serie A,
ikiwa na alama nne nyuma ya mabingwa watetezsi hao.
Mlinda
mlango huyo mzaliwa wa Brazil kwasasa akiwa QPR, amesisitiza kuwa klabu yake ya
zamani inapaswa kuingia katika mchezo huyo huku wakiondoa hofu dhidi ya bibi
kizee cha Turin.
Amenukuliwa
na Gazzetta dello Sport akisema,
"Juve lazima
ishambuliwe katika mchezo huo,kwanini wasishambuliwe? Inter anaonekana ndio
mpinzani mkubwa pengine mpinzani pekee. Inawezekana hata zaidi ya Napoli, ambao
hawako vizuri kama Inter.
"nilikuwa
nma muda wa kujifunza filosofia ya Andrea Stramaccioni, nilitaka kufanya naye kazi zaidi.
Ana njia nzuri ya kuona mchezo na kwa unyenyekevu ana msikia kila mtu lakini
hana woga.
Cesar aliondoka
Giuseppe Meazza majira ya kiangazi na nafasi yake ilichukuliwa na Samir
Handanovic, ambaye alitokea Udinese.
Robin van Persie awamaliza Arsenal.
Mshambuliaji
wa zamani wa washika mitutu wa England Robin van Persie hii leo alikuwa ni
mwiba mchungu kwa klabu yake hiyo ya zamani ya Arsenal, kufuatia hii leo
kuwafunga jamaa zake katika mchezo ulimalizika kwa Mashetani wekundu Manchester
United kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 mchezo ulipigwa katika dimba la Old
Trafford.
Ilimchukua
mduchi huyo dakika tatu kuandika bao la uongozi ukiwa ni mchezo wake wa kwanza
kucheza dhidi ya timu yake ya zamani ambayo aliihama kwa ada ya uhamisho wa
pauni milioni 24 majira ya kiangazi, kabla ya Wayne Rooney kukosa penati ambayo
pengine ingeandika bao la pili kwa United.
Patrice Evra
aliiandikia United bao la pili kunako dakika ya 66 ya mchezo bao ambalo ndilo
lilikuwa bao la ushindi ambalo limeipeleka moja kwa moja United katika uongozi
wa ligi ya soka nchini England maarufu kama ‘Premier League’ ndani ya muda
mfupi wakati yakisubiriwa matokeo ya mchezo kati ya Chelsea dhidi ya Swansea.
Arsenal ililazimika
kucheza ikiwa pungufu ya mchezaji mmoja katika dakika 21 za mwisho wa mchezo kufuatia
Jack Wilshere kutolewa nje ya uwanja
baada ya kupewa kadi ya pili ya manjano kabla ya Santi Cazorla kufunga goli la
kufutia machozi ukiwa ni mpira wa mwisho katika mchezo huo.
Mashabiki takribani
3,000 waliokuwa ndani ya Old Trafford jioni ya leo walikuwa wakionyesha hasira
zao waziwazi huku wakiimba nyimbo ambazo zilimlenga mtendaji mkuu wa Gunners Ivan
Gazidis kwa maneno ya ‘tunaitaka Arsenal yetu irejee’.
No comments:
Post a Comment