Al Hilal ya
sudan imejiweka katika mazingira mazuri ya kutinga hatua ya fainali ya kombe la
shirikisho barani Afrika baada ya jana kufanikiwa kuichapa Djoliba ya Mali kwa
mabao 2-0 katika mchezo wa kwanza wa michuano hiyo.
Mabao ya
Hilal yaliwekwa kimiani na Ibrahima Sane na Mudathir Careca.
Katika
kipindi cha miaka mitano iliyopita Hilal ilishindwa mara tatu kupenya katika
hatua hiyo katika michuano ya vilabu bingwa Afrika na mara moja katiki mochuano
ya kombe la shirikisho.
Walimaliza
katika nafasi ya pili katika kundi A na hivyo kujikuta wakikutana na Djoliba, ambao
waliibuka washindi wa kundi B.
AC Leopards watakuwa
wenyeji wa Al Merreikh katika mchezo wa nusu fainali nyingine itakayopigwa hapo
kesho.
No comments:
Post a Comment