KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, July 10, 2014

SERGIO ROMERO SHUJAA WA MCHEZO WA NUSU FAINALI YA PILI AIPELEKA ARGENTINA FAINALI WAKISUBIRI KWA MIAKA 24

Wao: Wachezaji wa Argentina wakitoka nduki kwenda kwa mfungaji wa penati ya nne na ya ushindi Maxi Rodriguez na wengine kwa mlinda mlango Sergio RomerO

Hizi ni nyuso za furaha kutoka kwa warembo wa Argentina baada ya matokeo ya ushindi wa penati
Mlinda mlango wa Argentina Sergio Romero amefanikiwa kudaka penati mbili za Ron Vlaar na kiungo mzoefu Wesley Sneijder na kuzima ndoto za Uholanzi kucheza fainali dhidi ya Ujerumani na kufanikisha ndoto za Lionel Messi

Argentina itakutana na Ujerumani katika fainali ya Kombe la Dunia baada ya kuibwaga Uholanzi kupitia mikwaju ya penalty. Lionel Messi na wenzake waliwafunga Waholanzi 4-2 baada ya mchezo kuisha 0-0

Mlinda lango wa Argentina Sergio Romero aliokoa penalty mbili na kuipa tikiti nchi yake kushiriki katika fainali ya Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza tangu mwaka wa 1990.
Mchezo huo ulikuwa kinyume kabisa na kivumbi ambacho Ujerumani iliimiminia Brazil magoli saba kwa moja katika nusu fainali ya kwanza. Lakini Romero, ambaye hakucheza mechi nyingi katika klabu yake ya Monaco msimu uliopita, alizuia penalty zilizopigwa na Ron Vlaar na Wesley Sneijder.

 Akizungumza baada ya miujiza yake, Romero alisema alikuwa na matumaini ya kuzuia penalty kadhaa na anamshukuru Mungu kuwa mambo yalimwendea sawa. Sasa anasema wameondoka uwanjani wakiwa na furaha na sasa kilichobaki ni kujiandaa sawa sawa kwa fainali. Ilikuwa ni mara ya pili kwa Uholanzi, ambao walishindwa na Uhispania katika fainali ya 2010, kuondolewa katika nusu fainali ya Kombe la Dunia kupitia matuta. Waliangushwa na Brazil mwaka wa 1998.

Arjen Robben mshambuliaji wa Uholanzi amesema walijitolea kwa moyo wote na anajivunia timu nzima. Aliongeza kuwa mchezo uliamuliwa na penalty na Wargentina wakafaulu, lakini kushindwa kwa njia hiyo inaudhi na inaumiza sana.
Matokeo hayo yalikuwa mabaya sana kwa Vlaar ambaye alikuwa imara katika ngome ya Uholanzi katika kipindi kizima cha mchezo kwa kuwanyamazisha washambuliaji wa Argentina.
 Messi hakuwa na jawabu lolote kutokana na mchezo mzuri wa beki huyo. Ijapokuwa mlinda lango Tim Krul aliokoa penalty mbili katika ushindi wa Uholanzi dhidi ya Costa Rica kwenye robo fainali, Kocha Louis van Gaal alikuwa na imani Jasper Cillessen mara hii. Lakini baadaye alikuja kujutia uamuzi huo, akisema kuwa hangeweza kufanya chochote kwa sababu alikuwa tayari amewatumia wachezaji wake watatu wa akiba.
Pia alijutia ukweli kwamba kipa wa Argentina Romero, alikuwa mwanafunzi wake wakati mmoja. Van Gaal alisema “bila shaka nilimfunza Romero namna ya kuzuia penalty kwa hivyo hilo limeniumiza”.
Romero aliokoa penalty za Vlaar na Snjeider na kuiweka Argentina katika nafasi nzuri, huku Messi, Ezequel Lavezzi na Sergio Aguero wote wakitikisa wavu. Ilikuwa zamu ya Maxi Rodriguez kupiga penalty ambayo iliwapeleka Argetina katika uwanja wa Maracana kwa fainali ya Jumapili dhidi ya Ujerumani.
Ulikuwa ni ushindi wa pili wa Argentina katika mechi tisa walizocheza na Uholanzi – na wao wa kwanza tangu fainali ya Kombe la Dunia la 1978 – na ulimwezesha Messi na wenzake kutoa heshima zao kwa gwiji wa Argentina Alfredo di Stefano, aliyeaga dunia Jumatatu mjini Madrid akiwa na umri wa miaka 88. Lakini kabla ya mpambano wa fainali, Uholanzi watashuka dimbani na Brazil siku ya Jumamosi kwa mchuano wa kumtafuta mshindi wa tatu.
 
Argentina sasa wanaelekea katika dimba la Maracana  kwa mchezo wa fainali dhidi ya Ujerumani Jumapili.
 
Swali katika penati ni kuwa je kulikuwa na nafasi kwa mlinda mlango wa akiba Tim Krul kurejesha ushujaa wake wa kudaka penati kama alivyofanya dhidi ya Costa Rica? jibu ni kuwa meneja wa Uholanzi Luis Van Gaal alikuwa ameshamaliza kuingiza idadi ya wachezaji mpaka muda wa nyongeza una malizika na hivyo jukumu likabaki kwa mlinda mlango wa mchezo wa dakika za uwanjani Jasper Cillessen, ambaye alibadilishwa katika robo fainali.
We're through! Argentina celebrate their moment of victory over Holland in the penalty shoot-out, as Maxi Rodriguez tucked away the winning kick
Tumepita tumepita! Argentina wakishangilia baada ya kuibwaga Uholanzi kwa penati huku penati ya mwisho ikipigwa na Maxi Rodriguez

No mistake: Maxi Rodriguez stepped up to convert Argentina's fourth penalty and send them through to a final with Germany
Bila kufanya makosa: Maxi Rodriguez akirejea kwa furaha baada ya kuitumbukiza wavuni penati ya nne iliyo wavusha Argentina mwenye fainali.Shoot-out hero: Sergio Romero saves Ron Vlaar's penalty as Argentina prevailed 4-2 in the shoot-out to reach the final
Shujaa wa penati mlinda mlango Sergio Romero akiokoa penati ya Ron Vlaar na kuandikisha ushindi wa Argentina

Party time: Lionel Messi leads the celebrations on the pitch at the Arena de Sao Paulo as Argentina made their first World Cup final in 24 years
Lionel Messi akiiongoza furaha na wachezaji wenzake uwanja Arena de Sao Paulo na Argentina wakiandikisha kutinga fainali ya kwanza katika kipindi cha miaka 24.

All over: Louis van Gaal will now turn his attentions to Manchester United after Holland's elimination
Tumekwisha Louis van Gaal akikuna kichwa ambapo sasa anarejea katika jukumu la kuinoa Manchester United baada ya kombe la dunia
Glimpse into the future? Argentina fans hold up a banner prophesying their side will be lifting the trophy on Sunday night
Mashabiki wa Argentina wakishikilia kitambaa kinacho hamasisha juu ya kikosi chao kuchukua taji la kombe la dunia
Hair-raising: Fans of Holland and Argentina in vibrant costumes assemble outside the Itaquerao Stadium ahead of the match
Hawa jamaa walipiga picha hii kabla ya mchezo sasa sijui baada ya mchezo kumalizika walipata wasaa wa kupiga picha nyingine kama hii