KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, August 18, 2014

Juan Cuadrado hana mpango tena wa kuelekea ngome kongwe



Nyota anayewindwa na Manchester United Juan Cuadrado ataendelea kusalia Fiorentina msimu huu wa uhamisho wa kiangazi hii ikiwa ni kwa mujibu wa meneja Vincenzo Montella.

Nyota huyo wa kimataifa wa Colombia amekuwa akihusishwa na kuelekea United na Barcelona, baada ya kuonyesha soka safi wakati wa fainali za kombe la dunia nchini Brazil.

Matumaini ya Man United kumkamata kiungo huyo yalionekana kupanda zaidi wiki iliyopita wakati Barca walipojiondoa katika harakati hizo na sasa inavyoonekana ni kuwa ataendelea kusalia nchini Italia.

‘Sikuwahi kufikiri kumpoteza Juan. Alikuwepo hapa hapo nyuma na sasa bado yupo na ataendelea kusalia hapa hapo baadaye’amesema Montella.

‘siadhani kama stori za Cuadrado zitakwisha.

‘Mchezaji wa aina yake anaweza kucheza katika kila eneo la kiungo.’

Wakati hayo yakiwa hivyo , Louis van Gaal bado naonekana kukaribia kusainisha Angel Di Maria,baada ya bosi wa Real Madrid Carlo Ancelotti kuonekana kuwa na mashaka na hatma ya baadaye ya winga huyo.

No comments:

Post a Comment