KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, August 18, 2014

Kuelekea mchezo wa Supercopa baina ya Real Madrid na Atletico Madrid, Simione anasema haoni utofauti kati ya timu hizo mbili

Kocha wa Atletico Madrid Simione anajiamini kuelekea mchezo wa Supercopa kesho
Bosi wa Atletico Madrid Diego Simione kwa mara nyingine tena ameendelea kuelelezea tofauti iliyoko baina ya kikosi chake na wapinzani wao wakubwa wa jiji la Madrid, Real Madrid, kuwa ni bajeti tu ya usajili.

Pande zote mbili zimetumia zaidi ya euro milioni €100 katika dirisha hili la uhamisho wa kiangazi, lakini mabingwa wa Hispania wakionekana kusajili wachezaji Antoine Griezmann na Mario Mandzukic ilhali James Rodriguez, Toni Kroos na Keylor Navas wakitua Bernabeu.

"Tuna wachezaji saba au nane kwa euro milioni €95" 
Simeone amewaeleza waandishi wa habari kabla ya timu hizo mbili kukutana katika mchezo wa kesho wa Supercopa.

"Kuna tofauti ndogo na siku zote klabu imekuwa na ubunifu. Tumejenga kundi, lakini si tu wachezaji 11, ni wachezaji 18 au 20."

Simeone akaendelea kwa kusema kikosi chake kitafanya vizuri hata bila ya Diego Costa, ambaye amejiunga na Chelsea kiangazi hii baada ya kuisaidia Atletico katika ligi kuu ya Hispania La Liga.

"Mfumo wa timu hautabadilika"
"Nia na madhumuni ni ile ile kwasababu inakuja kutoka kwenye kiini. Hiyo inatupa uimara kusonga mbelea na wazo hilo hilo"

Atletico ilipoteza taji la Supercopa de Espana msimu uliopita mbele ya Barcelona kwa goli la ugenini na Simeone mara hii angependa kufanya mabadiliko dhidi ya Madrid.

Atletico wanaelekea Santiago Bernabeu kwa mchezo huo wa kwanza hapo kesho Jumanne kabla ya mchezo wa marudiano utakaopigwa nyumbani kwa Madrid dimba la Vicente Calderon Ijumaa kupata maamuzi ya bingwa.