Mshambuliaji wa Yanga raia wa Brazil Geilson Santos Santana “Jaja” |
Klabu ya Itabaina FC ya nchini Brazil imekuwa ni kikwazo cha kufanikisha kupatikana kwa hati ya uhamisho wa kimataifa(ITC) ya mshambuliaji mpya wa klabu ya Yanga Geilson Santos Santana ‘Jaja’ mara baada ya mshambuliaji huyo kufanikiwa katika majaribio yake kwa watoto hao wa Jangwani.
Jaja ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu ya Yanga hataweza kutumiwa na klabu yake mpya mpaka hapo hati hiyo ya uhamisho wa kimataifa itakapo wasili nchini.
Akiongea na mtandao wa Rockersports.com, katibu mkuu wa Yanga Beno Njovu amesema klabu ya Itabania fc wamekuwa wagumu kutoa ushirikiano kwa kutoa barua ya kukubali kumtoa mshambuliaji huyo baada ya mazungumzo na wakala wake kwenda vizuri.
Amesema barua ya klabu yake za zamani ni lazima katika kufanikisha mchakato mzima wa uhamisho wa mchezaji huyo ambayo itawapa nafasi ya kuendelea na mchakato wa kupata ITC ya mshambuliaji huyo ambaye atakuwa ameungana na M-brazil mwenzake Andrey Couthino ambaye yeye ITC yake haikuwa na tabu kupatikana kwake.

Hata hivyo Njovu amesema klabu yake bado inaendelea na jitihada za ili kuhakikisha suala hilo linafakiwa kabla ya michuano ya Kombe la Kagame nchini Rwanda haijaanza.
'Inachukua kama siku nne au tano kukamilisha mchakato mzima wa kupata ITC, hivyo endapo klabu yake ya zamani itatoa 'reliese letter' tunaimani tutafanikiwa kabla ya Kagame Cup' amesema Njovu.
Bofya chini kumsikiliza katibu wa Yanga Beno Njovu
Yanga inatarajia kupeleka kikosi cha pili nchini Rwanda kwa ajili ya michuano ya Kagame ambayo inatarajiwa kuanza agosti 8 2014.
No comments:
Post a Comment