Balotelli alipanda Ferrari yake huko Brescia akijiandaa kwa safari ya kuelekea Liverpool |
Liverpool imempa Mario Balotelli kivutio kikubwa cha fedha kwa matumaini kuwa itasaidia katika kukidhi mahitaji yake pamoja na kujituma zaidi ndani ya Anfield.
Baada ya liverpool kukubali kutoa ada ya pauni milioni £16 kwa AC Milan na kushikilia mpango wao wa kukutana na wakala wa mchezaji huyo Mino Raiola, tayari Balotelli ameshakwea pipa kuelekea Manchester tangu jana kwa ajili ya vipimo vya afya na kukutana na ana kwa ana na meneja wa Liverpool Brendan Rodgers kwa mara ya kwanza.
Mamia ya mashabiki wa Liverpool walijitokeza kumlaki katika uwanja wa mazoezi wakati akiondoka ikiwa ni ishara kuwa ayapata mapokezi mazuri atakapo tua rasmi Anfield. endapo mambo yote yatakwenda vizuri mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Italia basi atasaini mkataba wa miaka mitatu utakao kuwa na thamani malipo ya kati ya pauni £85,000 mpaka £90,000 kwa wiki.
Lakini pamoja na hayo anatarajiwa kupata bonasi ya ambayo itakuwa ndani ya mkataba ambayo kimsingi itapelekea kumfanya asichomoe kuingia mkataba na klabu hiyo.
Balotelli amekutana na mashabiki nje ya uwanja wa mazoezi wa Liverpool wa Melwood baada ya mazungumzo ya uhamisho wake wenye thamani ya pauni milioni £16 akitokea AC Milan
Akiwa njiani: Balotelli akiondoka uwanja wa mazoezi wa Melwood baada ya mazungumzo ya hao jana Ijumaa
Mamia ya mashabiki wa Liverpool wakiwa wamekusanyika nje ya uwanja wa mazoezi kwa lengo la kujionea wenyewe mshambuliaji wao mpya Balotelli
Super striker: Balotelli akiwasili Melwood kwa mazungumzo baada ya kusafiri akitokea Italia kwa ndege binafsi
Inaarifiwa kuwa mkataba huo pia umeingizwa vifungu ambayo vitahusisha hatua za kidhamu ambazo zinaweza kuchukuliwa kwa mchezaji huyo endapo atakwenda kinyume.
Swali ni je Balotelli atajiepusha na matatizo? Lakini pia kipo kifungu ambacho kinaipa uwezo Liverpool kuchagua kumuongezea mwaka mmoja ndani ya mkataba wake huo.
Rodgers
amekataa kuulizwa maswali kuhusu Balotelli katika mkutano wake na waandishi wa habari lakini amesisitiza kuwa mazingira magumu aliyoyajenga kwa miaka miwili iliyopita ni imara kiasi kumuingiza kila mtu mpya ndani yake na kufanana nayo.
No comments:
Post a Comment