KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, September 5, 2014

Coastal Union ya Tanga kutambulisha wachezaji wake Septemba saba Mkwakwani 'Coastal Day'

Baadhi ya wachezaji wa Coastal watakao tambulishwa Septemba saba uwanja  wa Mkwakwani
UONGOZI wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga unatarajiwa kufanya utambulisho rasmi kwa wachezaji wote waliosajiliwa kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara unaotazamiwa kuanza kutimua
vumbi Septemba 20 mwaka huu.

Utambulisho huo utafanyika siku ya “Coastal Union day” ambayo hufanyika kila mwaka inapofika Septemba 7 mwaka huu ambao kufanyika
mchezo wa mpira wa miguu ambapo msimu huu Coastal Union itacheza na Polisi Morogoro kwenye uwanja CCM Mkwakwani.

Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga amesema kuwa maandalizi ya kuelekea utambulisho huo yamekamilikwa kwa asilimia kubwa.

Assenga amesema katika kuelekea siku hiyo maalumu kwa timu hiyo wataangalia uwezekano wa kucheza na timu itakayotajwa baadae baada ya
mazungumzo kumalizika.

"Siku hii itakuwa ni maalumu sana kwa timu yetu tunatarajia tutaweza kufanya jambo hilo kwa wanachama,wapenzi na mashabiki wetu ili waweze kufahamu kikosi chao kabla ya kuanza msimu mpya wa ligi kuu Tanzania bara"

Akizungumzia maandalizi ya kuelekea msimu mpya wa ligi kuu,Assenga amesema kuwa maandalizi kwa timu hiyo yanaendelea vizuri kwa wachezaji
kufanya mazoezi asubuhi na jioni.

No comments:

Post a Comment