KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, September 21, 2014

Ligi kuu ya Vodacom: Mabingwa watetezi wa taji Azam waifumua Polisi Tanzania


Azam FC imeanza vyema kampeni za kutetea ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara leo baada ya kuichapa Polisi Morogoro mabao 3-1 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Ushindi huo unaomfuta machozi kocha Mcameroon, Joseph Marius Omog baada ya kufungwa 3-0 na Yanga SC katika mchezo wa Ngao ya Jamii ulitokana na mabao ya Didier Kvumbangu mawili na Aggrey Morris.
Azam walikwenda kupumzika wakiwa wanaongoza mabao 2-0, Kavumbangu akianza kufunga dakika ya 14 akiunganisha pasi ya Kipre Tchetche katikati ya beki na kipa wa Polisi.
Beki Aggrey Morris akaipatia bao la pili Azam FC dakika ya 23 aliyemalizia mpira wa adhabu uliopigwa na Kipre Tchetche kufuatia beki Gardiel Michael kuchezewa rafu na Bantu Admin.
Baada ya mabao hayo mawili ya haraka haraka, kocha wa Polisi Morogoro, Mohammed Adolph ‘Rishard’ alimpumzisha kiungo Bantu Admin na kumuingiza James Mganda.
Mabadiliko hayo kidogo yaliituliza Polisi na kuanza kufika kwenye lango la Azam, ingawa hawakufanikiwa kupata bao hadi dakika 45 za kwanza zilipokamilika
Mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, Danny Mrwanda alidhibitiwa vikali na mabeki wa Azam leo.   
Kipindi cha pili, Azam FC ilirudi vizuri na kusukuma mashambulizi mfululizo langoni mwa Polisi, lakini mshambuliaji Kipre Tchetche alikosa mabao matatu ya wazi.
Nahoda Bakari aliipatia bao Polisi dakika ya 60 baada ya kuanzishiwa kona fupi na kumtungua kwa shuti la umbali 22 kipa Aishi Manula.
Didier Kavumbangu aliifungia bao la tatu Azam FC dakika ya 90 akimalizia krosi ya Farid Malik.
Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Aishi Manula, Shomary Kapombe, Gardiel Michael, David Mwantika, Aggrey Morris, Kipre Balou, Himid Mao/Khamis Mcha ‘Vialli’ dk72, Mudathir Yahya, Didier Kavumbangu, Kipre Tchetche/Farid Malik dk72 na Salum Abubakar.
PolisiMoro; Tony Kavishe, Rogeri Fred, Simon Fanuel, Ally FeruziTelu, LulangaMapunda, Said Jella, Bantu Admin/James Mgandadk22, NahodaBakari/SuleimanKassim‘Selembe’dk65, Danny Mrwanda, MachakuSalumna Nicholas Kabipe/Edgar Charles dk65

No comments:

Post a Comment