KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, September 20, 2014

YANGA YASHINDWA KUKAMUA MIWA YA MTIBWA YALAZIMISHWA KULA FUNDO MBILI UWANJA WA JAMHURI

Wakiwa ni wenye matumaini makubwa Yanga waliosindikizwa na mashabiki lukuki walijikuta wakikubali kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa wakata miwa wa Turiani Mtibwa Sugar inayonolewa na kocha Mecky Mexime.

Mabao ya Mtibwa katika mchezo huo uliokuwa wa kasi kwa dakika zote 90 yaliwekwa kimiani na mshambuliaji wa zamani wa Simba na timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Mussa Hassan 'Mgosi' kwenye dakika ya 15 wakati msumari wa pili ukishindiliwa kimiani na Ali Ame kwenye dakika ya 83.

Katika mtanange huo pia ulishudia mshambuliaji pendwa katika kikosi cha Yanga Geilson Santos Jaja akikosa penati kwenye dakika ya 46 ya kipindi cha pili cha mchezo iliyopanguliwa na kipa wa Mtibwa Said Mohammed.

Yanga walionekana kuutawala mchezo huo kwa kipindi kirefu lakini Mtibwa walionekana kunufaika zaidi na mipira ya 'counter Attack' mashambulizi ya kushtukiza yaliowapa mabao yao mawili kwa njia nyepesi.