KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, September 24, 2014

Luis Van Gaal kumrejesha Gerrard Pique usajili wa Januari

Mlinzi wa Barcelona Gerard Pique kurejea Old Trafford?
Imeripotiwa kuwa Manchester United wana mpango wa kumrejesha Gerard Pique Old Trafford akitokea Barcelona.
Mlinzi huyo aliondoka United mwaka 2008 kwa uhamisho uliogharimu pauni milioni £5 ambapo amekuwa mchezaji wa kutumainiwa Katalunya tangu wakati huo ambapo ameisaidia kutwaa mataji manne ya ligi ya Hispania 'La Liga' mataji mawili ya ligi ya mabingwa Ulaya na mawili ya Copa del Reys.
Hata hivyo nyota huyo wa kimataifa wa Hispania mpaka sasa ameitumikia timu yake michezo mitatu tu huku bosi mpya wa Barcelona Luis Enrique akionekana kupendelea zaidi kumtumia Javier Mascherano na Jeremy Mathieu katika sehemu ya ulinzi.
Kwa mujibu wa gazeti moja la nchini Hispania la AS limearifu kuwa Manchester United inataka kutumia mwanya huo kuweka pendekezo la kutaka kumsajili Pique kurejea Old Trafford, licha ya kwamba mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 27 akiwa ndio kwanza amesaini mkataba wa nyongeza na Barca.
Bosi Louis van Gaal kwasasa analazimika kusaka namna ya kuimarisha eneo la ulinzi katika kikosi chake mwezi Januari wakati huu ambapo United ikiwa imekusanya alama tano tu katika michezo mitano tangu kuanza kwa msimu mpya wa Premier League huku ikiwa tayari imeshatolewa katika kombe la Capital One na MK Dons.