Kocha Maximo wa Yanga akiwa na Jerson Tegete aliyerejea kikosini baada ya kufanikiwa kuponya majeraha yake |
Kikosi cha timu ya Young
Africans kitashuka dimba la Uwanja wa Taifa siku ya jumapili kupambana
na Wajela Jela timu ya Jeshi la Magereza nchini Prisons FC kutoka jijini
Mbeya ikiwa ni mchezo wa pili wa mzunguko wa Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania bara msimu
wa 2014/2015.
Akiongea na tovuti rasmi ya
klabu leo mara baada ya mazoezi, kocha mkuu wa Young Africans mbrazil
Marcio Maximo amesema vijana wake wako fit kuelekea mchezo huo wa siku
ya jumapili huku wakiwa wamejipanga kuhakikisha wanaondoka na pointi
tatu muhimu.
Maximo amesema baada ya
kupoteza mchezo wa awali dhidi ya wakata miwa wa Mtibwa Sugar, kikosi
chake kimekua kikiendelea na mazoezi kila siku katika uwanja wa shule ya
sekondari Loyola huku wakiyafanyia marekebisho makosa yaliyojitokeza
katika mchezo huo
wa awali.
Kiungo Coutinho apona majeraha yake |
Kuhusu timu ya Tanzania
Prisons mbrazil Maximo amesema anatambua walishinda mchezo wa awali
dhidi ya Ruvu Shooting hivyo wana morali bado ya kuendeleza ushindi siku
ya jumapili, lakini pia kikosi changu kipo fit kwa mchezo huo kwa
kusaka pointi tatu muhimu.
Aidha Maximo amesema habari
njema kwa wana Yanga ni kurejea dimbani kwa kiungo Andrey Coutinho
pamoja na mshambuliaji Jerson Tegete ambao wanatarajiwa kuonekana kwenye
mchezo huo na kuhakikisha wanaisaidia timu yao kupata ushindi.
Wachezaji watakaoukosa mchezoa
wa siku ya jumapili ni Oscar Joshua na Hussein Javu ambao wote ni
majeruhi, wakisumbuliwa na maumivu ya nyama za paja, na jumatatu
wanatarajiwa kuanza mazoezi mepesi baada ya kuwa kwenye matibabu chini
ya usimamizi wa daktari
wa timu Dr Suphian Juma.
Mwisho kocha Marcio Maximo
amewaomba wapenzi, washabiki, wanachama na wadau wa soka kwa ujumla
kujitokeza kwa wingi siku ya jumapili katika mechi dhidi ya Prisons kuja
kuwapa sapoti vijana na kuwashangilia muda wote wa mchezo.
No comments:
Post a Comment