Mshambuliaji wa Simba Emanuel Okwi akikokota mpira huku mchezaji wa Jacob Massawe akimnyemelea wakati wa mechi ya ufunguzi wa ligi ambapo Simba ilishinda bao 3-0. |
Ligi kuu ya Tanzania Bara imeanza hii katika viwanja saba tofauti hapa nchini , ambapo mabingwa watetezi wa taji, Simba walikuwa katika uwanja wa taifa ikifungua pazia la ligi dhidi ya Afrikan Lyon imechomolza na ushindi wa mabao 3-0.
Simba imepata mabao yake kupitia kwa mshambuliaji hatari Emmanuel Okwi bao lililopatikan katika kipindi cha kwanza kabla ya bao la pili kuwekwa wavuni na mlinzi wa kulia Nassoro Cholo.
Bao la tatu lilipatikana katika kipindi cha pili kupitia kwa njia ya penati baada ya walinzi wawili wa Lyon kumkwatua Emmanuel Okwi katika eneo la hatari na bao hilo kuzamishwa wavuni na mshambiliaji Daniel Akufor.
Mara baada ya mchezo huo kumalizika kocha wa Simba Milovan Circkovic amesema ameridhishwa na kiwango cha timu yake huku akipongeza kikosi chake kwa kuanza ligi hiyo na matokeo hayo.
Amesema anatarajia nidhamu ya kimchezo iliyoonyeshwa na kikosi chake itaendelezwa katika mchezo unaofuata ambao Simba itakuwa ikicheza dhidi ya JKT Ruvu mchezo ambao utapigwa katika uwanja wa Taifa.
Matokeo mengine mabingwa wa kombe la Kagame Yanga wamekwenda sare ya bila mabao 0-0 na Tanzania Prisons mchezo uliopigwa katika uwanja wa Sokoine pale mkoani Mbeya.
MATOKEO MENGINE
Yanga 0 vs 0 Tanzania Prisons
Simba 3 vs 0 Afrikan Lyon
Mgambo JKT 0 vs 1 Coast union
Toto Afrikan 1 vs 1 JKT Oljoro
Kagera Sugar 0 vs 1Azam fc
Ruvu Shooting 1 vs 2 JKT Ruvu
Polisi Moro 0 vs 0 Mtibwa Sugar
RATIBA MZUNGUKO WA PILI
| ||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
No comments:
Post a Comment