Ronaldo Di
Lima amesema kuwa nyota wa Barcelona ya Hispania Lionel Messi ndiye anaye
mvutia zaidi na mzuri zaidi ukimlinganisha na mshambiliaji wa Real Madrid
Cristiano Ronaldo, kwa kuwa Messi ni
mbuni katika kutafuta nafasi.
Wachezaji hao
wawili wa ligi ya Hispania ‘Primera Division’ wamekuwa wakionekana kama wachezaji
bora kwasasa duniani na Di Lima anasema Ronaldo anapaswa kumpigia saluti Messi
licha ya kuvutiwa na Ronaldo kwa aina ya uchezaji wake.
Akinukuliwa na
CNN amesema
"Messi yuko
juu zaidi ya Cristiano Ronaldo kwa maoni yangu, licha ya kwamba anatokea Argentina,
taifa ambalo ni wapinzani wakubwa wa Brazil. Lakini nawapenda wote."
No comments:
Post a Comment