Meneja wa Manchester
City Roberto Mancini kwa mara nyingine tena ameonyesha kushangazwa kwake na
sheria za shirikisho la soka Duniani FIFA kufuatia hivi karibuni kuiitwa katika
timu ya Taifa kwa mshambuliaji wake aliye majeruhi Sergio Aguero, na kuziita
sheria za FIFA kuwa ni za kipumbavu.
Aguero amekuwa
nje ya uwanja kufuatia maumivu ya mguu tangu mchezo wa kwanza wa ufunguzi wa
msimu wa ligi kuu ya England ‘Barclays Premier League’ ambao City walikuwa
dimbani dhidi ya Southampton wiki nne zilizopita.
Lakini licha
ya mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24 kutakiwa kuwa nje ya dimba mpaka mwishoni
mwa juma hili, hilo halikumzuia kocha wa Argentina Alejandro Sabella kumwita katika
kikosi chake kwa ajili ya michezo miwili ya kampeni ya kuwania kucheza fainali
ya kombe la dunia dhidi ya Paraguay na Peru.
Mancini amekubali
kuwa kocha huyo alikuwa na haki ya kumwita kikosini lakini kwa kumfanyia uangalizi
wa matibabu yake kwa mujibu sheria za bodi ya utawala ya fifa, lakini hawakuona
hilo kama lingemsaidia na kumpa nafuu mchezaji huyo.
Alipoulizwa kama
Aguero amesalia katika klabu yake katika
kipindi cha kufanyika michezo hiyo Mancini alijibu “Hapana, meneja wake alimtaka, na atakuwa huko
kwa siku tano, alifanyiwa uangalizi na wataalam, meneja alimtaka“.
“Hii ni
sheria ya kipuuzi kwasababu , kama tuna mchezaji ambaye ni majeruhi kwa wiki
mbili , ni vema akasalia hapa.”
Mancini ameielezea
sheria hiyo kama ni sheria ya kuchekesha pale aliposikia kuwa Aguero ameitwa katika
timu ya taifa, ambapo hapo kabla alitegemea kuwa mchezaji huyo angeruhusiwa
kubakia England.
Pamoja na
hilo, Aguero alitakiwa kufanyiwa kipimo cha afya yake leo kabla ya mchezo dhidi
ya Stoke.
Mchezaji huyo
aliyejiunga na City kwa ada ya uhamisho wa pauni milioni £38, alianza mazoezi
tena mapema wiki hii huku tayari kukiwa na matumaini ya kuwepo dimbani katika
mchezo utakao pigwa Britannia.
No comments:
Post a Comment