Sehemu ya mashabiki wa Colombia wakati wa kuipokea timu yao ikirejea kutoka Brazil |
Timu ya taifa ya Colombia iliondolewa kwenye fainali za
kombe la dunia katika hatua ya robo fainali baada ya kufungwa mabao mawili kwa
moja dhidi ya wenyeji timu ya taifa ya Brazil.
Mashabiki wa soka nchini Brazil wametangaza uadui wa maisha
na beki wa pembeni wa tyimu ya taifa ya Colombia Juan Zuniga, baada ya
kuchuikizwa na rafu aliyomfantyia mshambuliaji wake Neymar Da Silva Junior.
Mashabiki wa soka nchini Brazil wamethibitisha kwa vitendo
vita yao dhidi ya beki huyoa mbae anaitumikia klabu ya Societa Sportiva Calcio
Napoli ya nchini Italia kwa kuchana hadharani karata zenye picha yake.
Mashabiki hao wamesema katu hawawezi kumsamehe Zuniga,
kutokana na kosa alilowafanyia la kumuumiza muokozi wao ambapo aliamini
angefanikisha kila jambo walilolikusudia.
Hata hivuyo mashabiki hao wamelitaka shirikisho al soka
duniani FIFA kutoa adhabu kali kwa Juan Zuniga, kutokana na kuamini kwamba limcheza
rafu kwa makusudi dhidi ya Neymar.
Tayari imeshaelezwa kwamba Neymar hatocheza tena katika
michezo ya kombela dunia iliyosalia baada ya kuonekana amepata majeraha katika
sehemu ya mfupa unaoshikilia uto wa mgongo.
Neymar atuma salamu kwa wenzake waliosalia kikosini
Wakati huo huo Neymar amesema wachezaji wenzake bado wana
nafasi kubwa ya kumsaidia kutimiza ndoto ya kutwaa Kombe la Dunia.
Neymar atuma salamu kwa wachezaji wenzake |
Huku akimwaga machozi, Neymar amesema kuumia kwake hakuwezi
kuwa mwisho wa ndoto zake na Brazil kutwaa Kombe la Dunia
“Nafasi ipo, ninawaamini wenzangu wanaweza kufanya jambo na
kutimiza ndoto.
“Mimi nilikuwa ni sehemu ya timu, hivyo bado timu ina uwezo
wa kutimiza malengo yetu.
“Nawatakia wenzangu wote kila la kheri ili wafikie ndoto
zetu,” alisema.
No comments:
Post a Comment