KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, September 7, 2014

MAVETERANI WAMUENZI GEBO PETER KWA BONANZA (TEMBELEA MWAISABULA BLOG)

Pichani ni mkongwe Mao Mkami Ball Dansa akifanya yake kwa mbali ni Maalim Saleh 'Romario'


Pichani ni mratibu wa bonanza Richard Msungu
LILE BONANZA kubwa linalofanyika kila mwisho wa mwezi  linalohusisha wanasoka wa zamani waliowahi kutamba katika medani ya soka nchini limefanyika leo katika viwanja vya shule ya msingi Buguruni ambapo kwa mwezi huu lilikuwa la lengo la kumuenzi marehemu Gebo Peter.

Akizungumza na MWAISABULA BLOGU mratibu wa Bonanza ambaye pia ni kiongozi wa Uhuru Veteran Dr Richard Msungu amesema kuwa Bonanza la mwezi huu limejumuisha timu 8 tofauti na awali ambavyo lilikuwa likishirikisha timu 5.

Pia Msungu alitoa wito kwa maveterani wengine kujitokeza kwa wingi katika kushiriki katika Mabonanza kwani ni nafasi nzuri yao wao kujenga afya zao.

Bonanza hilo limedhaminiwa na hoteli ya LEKAM ROYAL LODGE & PUB iliyopo maeneo ya Buguruni.
Pichani ni baadhi ya wakongwe wakiongozwa na Kenny Mwaisabula (mzazi)

No comments:

Post a Comment