KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, September 5, 2014

Paul Scholes ana wasiwasi na meneja Luis Van Gaal juu ya safu ya ushambuliaji ya United

Atakaa wapi? Radamel Falcao akipiga picha na meneja msaidizi Ryan Giggs baada ya kusaini kwa mkopo katika siku ya mwisho ya usajili wa kiangazi
Paul Scholes ana wasiwasi wa Van Gaal kuwatumia washambuliaji wawili badala ya watatu baada ya kuwasili kwa Radamel Falcao
Kiungo wa zamani wa Manchester United Paul Scholes haoni ni kwa vipi meneja wa klabu hiyo Louis van Gaal atawatumia washambuliaji watatu Wayne Rooney, Robin van Persie na ngizo jipya Radamel Falcao katika timu moja.

Scholes anaamini kuwa Falcao, aliyejiunga na klabu hiyo kwa mkopo akitokea Monaco katika siku ya mwisho ya kufungwa kwa dirisha la usajili ni mchezaji wa aina ya pekee lakini anasisitiza kuwa klabu yake hiyo ya zamani itafanikiwa tu kuwatumia washambuliaji wawili tu kati ya washambuliaji watatu wenye majina.

Ameandika kupitia ukurasa wake katika gazeti la The Indepandent 
'Nilipokuwa nikimuona Falcao akiichezea Porto, Atletico Madrid na Monaco niliona ni mshambuliaji mwenye uwezo mkubwa na mwenye rekodi ya ufungaji tofauti kabisa katika dunia hii.

Who will miss out? Paul Scholes doesn't believe Louis van Gaal can field all three of his star strikers
Nani atakalia benchi? Paul Scholes haamini kama Louis van Gaal ataweza kuwatumia washambuliaji wote watatu kwa wakati mmoja.

'Falcao anaibua ushindani mkubwa katika safu ya ushambuliaji ya United. Hakuna namna ya kufanya kwa Van Gaal ya kuwachezesha wote kwa pamoja Rooney, Van Persie na Falcao. Itakuwa wawili kati ya watatu hao jabo ni ngumu kusema kwasasa.'
Scholes anaamini usajili wa mapesa na kuvutia wa klabu hiyo kiangazi ambao umewaleta Luke Shaw, Ander Herrera, Marco Rojo, Angel di Maria na Danny Blind ndani ya Old Trafford kwa jumla ya pauni milioni £150 umempa Van Gaal kikosi cha ushindi wa taji msimu huu kama si kumaliza katika nne za juu.

'Credit ziende kwa makamu mtendaji mkuu wa United Ed Woodward, ambaye amemuachia Van Gaal kikosi ambacho kinaweza kumaliza katika nafasi nne za juu," Amesema Scholes. 

'Sidhani kama ushindi wa taji la ligi ni lazima lakini katika Champions League ni dhumuni kuu. Sasa imebaki kwa Van Gaal kutengeneza kikosi.

Licha ya kufurahishwa na ujio wa wacheza wapya, Scholes amesema amehuzunishwa na kuondoka kwa mtoto aliyekulia Old Trafford (academy graduate) Danny Welbeck kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni £16 ambaye ameelekea Arsenal hata kama hawezi kufunga magoli 20 katika msimu.
'Danny hawezi kufikisha magoli 20-25 ndani ya msimu lakini anaweza kuifungia Arsenal magoli 10 mpaka 15.' 
Great expectations: The arrival of players like Angel di Maria have set United up for a top four finish
Matarajio makubwa: Ujio wa wachezaji kama Angel di Maria kumeifanya United kuwa na matumaini ya kumaliza katika nne bora
Not prolific: Danny Welbeck will not score 20 goals a season for Arsenal, warns Paul Scholes
Danny Welbeck